POLISI WANAWAKE ARUSHA WASHEHEREKEA PASAKA NA WATOTO YATIMA 
Kuelekea sikukuu ya Pasaka, Askari Polisi wanawake kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mkaguzi msaidizi wa Polisi Herieth Frank wametoa zawadi mbalimbali kwa kituo cha kulea watoto yatima cha Habashabi Orphanage Center kilichopo Kisongo Mkoani Arusha ikiwa ni sadaka yao kwa watoto.

Akiongea na watoto katika kituo hicho mkaguzi msaidizi Herieth amesema pamoja na majukumu yao ya kazi, huwa wanashirikiana na jamii katika matukio mbalimbali ya shida na raha ambapo ametoa wito kwa jamii kuendelea kuwasaidia watoto wanaoshi katika vituo vya kulea yatima.

Kwa upande wake Mkurungenzi wa kituo hicho Bi. LETICIA JULIUS ametoa shukrani kwa moyo wa upendo ulionyeshwa kwa watoto toka jeshi la Polisi kupitia Askari wanawake wa kikosi cha usalama barabarani.

Naye Dai Mayenga kwa niaba ya watoto waliopo katika kituo hicho ameshukuru kwa sadaka hiyo ambapo amesema waendelee na moyo huo huo wa upendo kwani Mungu ataendelea kuwaongezea pale walipotoa.

Akitoa historia fupi ya kituo hicho Mlezi wa Watoto Bi. Helen Mhina amesema kituo hicho kilianza rasmi mwezi Novemba 2015 kikiwa na jumla ya watoto wanne. Aliendelea kusema hadi hivi sasa kituo hicho kina watoto 22 na wote wanasoma shule za msingi na sekondari.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post