OJADACT, ERC WATAKA WAANDISHI WA HABARI WA TANZANIA KUFANYA KAZI NA WAANDISHI WA NCHI JIRANI KWENYE SEKTA YA MAZINGIRA

Mkutano ukiendelea mtandaoni

Na Mwandishi wetu Mwanza Tanzania

Chama cha waandishi wa habari wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania (OJADACT) kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la  Environmental Reporting Collective (ERC) Kwa pamoja wamewataka waandishi wa habari wa Tanzania kushirikiana kufanya kazi za uandishi wa habari za uchokonozi kwa pamoja na waandishi wa Nchi jirani kwenye eneo la uhalifu wa mazingira.

Mkurugenzi wa ERC Bwana Ian Lee amezungumza hayo kwenye ufunguzi wa mafunzo ya namna ya kiripoti habari za uhalifu wa mazingira yaliyofanyika leo kwa njia ya mtandao.

Bwana Lee alisema kuwa, shirika lake lina fungu la fedha kwa ajili kuwapa waandishi wanaotoka kwenye Nchi mbili tofauti walio na dhamira ya kufanya uchunguzi wa uhalibifu wa mazingira unaogusa Nchi zote mbili.

"Tunaelewa kuwa kuna changamoto ya fedha za kufanya uchunguzi ndio maana tumetenga fungu maalumu la kuwasaidia waandishi wenye dhamira ya kuandika masuala ya uhalibifu wa mazingira", alisema Lee.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa OJADACT  Bwana Edwin Soko alilipongeza shirika la ERC na pia kuwataka waandishi wa habari wa Tanzania kuchangamkia fursa hiyo.

Pia Soko aliongeza kuwa, uhalifu wa kimazingira ni hatari kwa ustawi wa Dunia hivyo waandishi watumie mafunzo hayo kupata ubobezi wa kuandika habari za mazingira.

Mafunzo hayo ya kimtandao ya siku moja yalijumuisha zaidi ya waandishi wa habari hamsini toka Mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.

Mafunzo hayo ya leo yalitanguliwa na mafunzo mengine yaliyofanyika April 2, 2022 yaliyojumuisha waandishi wa habari ishiriki na kufanyika katika Ukumbi wa Nyakahoja Jijini Mwanza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post