Picha : KIJANA ATEMBEZEWA KICHAPO, AOGESHWA MATOPEKijana huyo akiogeshwa matope
Kijana ambaye hajafahamika haraka jina lake anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 mpaka 30 mkazi wa Igoma halmashauri ya mji wa Njombe amenusurika kifo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali katika mtaa wa Mpechi eneo la Lutilage mara baada ya kukamatwa akiwa ameiba vitu mbali mbali ikiwemo TV,Godoro,Blanketi na Mtungi mdogo wa gesi.

Luo Lameck Mgeni ni mzee aliyekuwa amempangisha awali katika nyumba yake kabla ya kumfukuza kutokana na tabia ya wizi anasema anashangaa kuona kijana huyo ameondoka kwake lakini amerudi na kuiba kwenye moja ya nyumba ya familia yake.

“Leo nikasikia kule nyumbani wamebomoa nikauliza wameiba nini,kuingia mle ndani tukaona tandiko halipo na vitu vingine amechana chana ameweka nje”,amesema Mzee Mgeni.

Hata hivyo kabla kijana huyo hajafikiwa na hali mbaya kutokana na kipigo,Polisi wamefika na kufanikiwa kumuondosha katika eneo hilo.

CHANZO - MICHUZI BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post