Picha : MAHAFALI YA 10 KIDATO CHA SITA SHULE YA SEKONDARI MWENDAKULIMA YAFANYIKA...TCRA YAWATAHADHARISHA 'KUPOST' PICHA MTANDAONI

Wahitimu wakiandamana kuelekea ukumbini wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.

***
 Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mahafali ya 10 ya Kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo katika Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga yamefanyika leo Ijumaa Aprili 1,2022 ambapo jumla ya Wanafunzi wa kike 178 wanahitimu Elimu ya Kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Mwendakulima.

Akizungumza wakati wa Mahafali hayo, Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Magare Company Ltd, Mabula Magangila  amewaomba wazazi na walezi kushirikiana na walimu katika kulinda nidhamu ya wanafunzi na kuhakikisha wanahamasisha wanafunzi kwenda shule.

Magangila ameahidi kushirikiana na shule hiyo katika ujenzi wa uzio wa shule ili ujenzi uanze mara moja ili wanafunzi waishi salama huku akiahidi kutoa zawadi kwa walimu na wanafunzi watakaofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa.

“Naipongeza shule hii kwa kuendelea kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa lakini pia mnajitahidi sana katika utunzaji mazingira, shule ina miti mingi, inapendeza. Nawapongeza pia wadau wanaoshirikiana na shule hii kuondoa changamoto zilizopo na sisi Kampuni yetu ya Magare ni wadau wazuri wa sekta ya elimu na afya tunaahidi kutoa ushirikiano katika shule hii ikiwemo katika huu ujenzi wa uzio wa shule”,amesema.

Amewataka wahitimu hao kwenda kudumisha nidhamu waliyopata shuleni huko mtaani na pindi watakapokwenda Vyuoni wasiende kucheza bali wakajitume kwenye masomo yao.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Mwendakulima, Mjumbe wa Bodi hiyo ambaye pia Mlezi wa Wanafunzi wa shule hiyo, Mhandisi Francis Mihayo amewasihi wahitimu hao kuwa makini na matumizi ya Mitandao ya Kijamii.

“Mkishamaliza masomo yenu ya Sekondari mtaanza kumiliki hizi Simu Janja ‘Smartphones’, sasa kuweni makini sana na matumizi ya hizi simu za kupanguza”,amesema Mhandisi Mihayo ambaye ni Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa.

“Tatizo linaanzia pale mkianza chuo, mtakuwa na hizi simu za kupangusa na Kompyuta (Laptop) mkazitumie vizuri, msije mkaanza kutafuta Degree mkiwa na matatizo ya kuwa na picha chafu mtandaoni. Tatizo kubwa lililopo kwa wanafunzi wa Vyuo ni kuweka picha mtandaoni bila kujua madhara ya kufanya hivyo”,ameeleza.

“Lazima muwe makini na Matumizi ya mitandao ya kijamii. Ukishapiga picha na kupost mitandaoni kumbuka kile unachoweka kule kinabaki milele huko mtandaoni. Naomba mnapopiga picha muishie tu kupiga , msiweke picha mtandaoni. Pigeni picha lakini msiziweke mtandaoni bila kujua madhara yake”,ameongeza Mhandisi Mihayo.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwendakulima Neema Daniel amesema Jumla ya wanafunzi wa kike 178 wanamaliza elimu ya Kidato cha sita mwaka 2022 katika shule ya Sekondari Mwendakulima mwaka huu 2022.

Amesema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2017 ambayo sasa ina wanafunzi wa kike na wa kiume kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na wanafunzi wa kike pekee kwa kidato cha tano na sita ina jumla ya wanafunzi 1527.

Amebainisha kuwa ufaulu katika mitihani katika shule hiyo iliyopo jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi umekuwa ukiongezeka kila mwaka kutokana na miundombinu na mazingira rafiki ya kujifunzia kwa wanafunzi.

Amezitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo kuwa ni Viti 20 na meza kwa walimu na upungufu wa matundu ya vyoo kwa wanafunzi pamoja na ukosefu wa uzio hali  inayohatarisha usalama wa  wanafunzi lakini pia miundo mbinu ya shule akibainisha kuwa mahitaji yao sasa ni mchanga na nondo ili ujenzi wa uzio uanze mara moja.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Magare Company Ltd, Mabula Magangila ( wa pili kushoto) akijiandaa kukata utepe wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima. Katikati ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwendakulima Neema Daniel akifuatiwa na Mjumbe wa Bodi ya Shule ya Sekondari Mwendakulima na Mlezi wa wanafunzi, Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Zoezi la kukata utepe likiendelea wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wahitimu wakiandamana kuelekea ukumbini wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wahitimu wakiimba wimbo wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wahitimu wakiimba wimbo wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Magare Company Ltd, Mabula Magangila akizungumza wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Magare Company Ltd, Mabula Magangila akizungumza wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwendakulima Neema Daniel akizungumza wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.

Mjumbe wa Bodi ya Shule ya Sekondari Mwendakulima na Mlezi wa Wanafunzi shule hiyo, Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa akizungumza wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.

Wahitimu wakijiandaa kukabidhi zawadi ya Chupa ya chai, vikombe na sahani kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwendakulima Neema Daniel wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wahitimu wakikabidhi zawadi ya Chupa ya chai, vikombe na sahani kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwendakulima Neema Daniel wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Meza kuu wakifuatilia matukio wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.

Wahitimu wakisoma taarifa ya habari wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wanafunzi wakionesha Fasheni ya mavazi wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wanafunzi wakionesha Fasheni ya mavazi wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wageni waalikwa wakifuatilia matukio wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wanafunzi wakicheza nyimbo za asili wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mwendakulima wakitoa burudani ya 'Live Band' wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Mjumbe wa Bodi ya Shule ya Sekondari Mwendakulima Mhandisi Francis Mihayo ambaye ni Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa akimpa zawadi mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwendakulima baada ya kukoshwa na upigaji wake mzuri wa Gitaa.
Wanafunzi wakitoa burudani wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Igizo likiendelea wakati wa Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Walimu naa Wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wazazi na wageni waalikwa wakicheza na wahitimu kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Mhitimu Getrude Mayai akisoma risala kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wanafunzi wakitoa burudani ya Igizo kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Burudani ikiendelea kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Burudani ikiendelea kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima

Wanafunzi wakitoa burudani kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima
Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Magare Company Ltd, Mabula Magangila akikabidhi cheti kwa Mhitimu kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.

Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Magare Company Ltd, Mabula Magangila akiendelea kukabidhi vyeti kwa wahitimu kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.
Zoezi la kugawa vyeti kwa wahitimu likiendelea kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima
Meza kuu wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye Mahafali ya 10 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari Mwendakulima.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post