WANANCHI BUTIAMA WAHAMASISHWA KUTUNZA MIUNDOMBINU YA MAJI

Mradi wa maji kijiji cha Biatuka
Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) wilaya ya Butiama Mhandisi Mafuru Dominico

Na Dinna Maningo, Butiama

SERIKALI imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maji lakini baadhi ya wananchi wilaya ya Butiama mkoani Mara wamelalamikiwa kuharibu Miundombinu ya maji jambo linalorudisha nyumba mendeleo ya jamii.

 Hayo yalielezwa na Meneja Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA),Mhandisi Mafuru Dominico wakati waandishi wa habari walipotembelea mradi wa maji kijiji cha Biatuka kata ya Buhemba.

Dominico alisema kuwa baadhi ya vijiji vilivyojengewa mradi wa maji,wananchi wamekata mabomba ukiwemo mradi wa maji wa Bukabwa,Kamgendi na Kitaramanka.


 "Uharibifu unapofanyika kwenye miundombinu ya maji unasababisha kuongezeka kwa gharama za matengenezo fedha ambazo zingetumika kujenga miradi mingine,ukiharibu miundombinu ni lazima utatumia fedha zingine kutengeneza mradi, fedha ambazo zingefanya kazi nyingine hii hali inarudisha nyuma maendeleo maana ukikata bomba maji yatavuja na kupotea bure itabidi utumie fedha nyingine kufanya matengenezo", alisema Dominico.

 Alisema changamoto nyingine ni baadhi ya wananchi kufanya shughuli za kilimo kwenye maeneo ya vyanzo vya maji na kuchunga mifugo jambo linaloathiri vyanzo vya maji nakusababisha kupungua kwa maji kwenye vyanzo vya maji.

 Akizungumzia fehda za mradi Mhandisi huyo alisema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2021|2022 serikali imetoa fedha kutekeleza miradi saba ya maji katika wilaya hiyo kiasi cha sh Bilioni 2;4,vijiji vilivyopewa miradi ni kijiji cha Biatika kata ya Buhemba,Nyasirori kata ya Masaba,mradi wa Uviko-19 kijiji cha Nyamikoma kata ya Kyenyari,kijiji cha Mwibagi kata ya Kyenyari,Buswahili kata ya Buswahili,Kyankoma kata ya Nyamimange na mradi wa uboreshaji wa visima vya pambu ya mikono kwa kufunga sora za umeme katika vijiji vinne ambavyo ni kijiji cha Mmazami,Kyatungwe,Masurura na Nyambili.

Dominico alisema kuwa mradi wa Biatika umetengewa fedha Milioni 663,hatua za ujenzi zinaendelea na tenki la maji lenye ujazo wa lita 135,000 limekamilika kazi iliyopo ni uchimbaji wa mitaro,ulazaji wa mabomba na kuna vituo 25 vilivyojengwa kutoa maji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments