WAKULIMA WA PAMBA WASHAURIWA KUFUATA MATUMIZI SAHIHI YA VIUATILFU


Wakulima wa zao la pamba wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu wameshauriwa kufuata matumizi sahihi ya viuatilifu vya pamba ili kukabiliana na wadudu waharibifu wa zao hilo.


Ushauri huo umetolewa na barozi wa zao la pamba nchini Agrey Mwanri alipokuwa akitoa mafunzo ya namna ya kutumia viuatilifu pamoja na upuliziaji wa viuatilifu katika mimea ya pamba yaliyofanyika leo March 4, 2022 katika mji wa Bariadi mkoani hapa.

Mwanri amesema kushamiri kwa wadudu katika mimea ya pamba inasababishwa na matumizi ya viuatilifu yasiyo sahihi yaliyokithili kwa baadhi ya wakulima hali inayosababisha usugu wa madawa kwa wadudu na kushindwa kuwaathiri.

"Hii ni vita dhidi ya wadudu na inahitaji umakini ili kuwashinda wadudu hawa tukishindwa kuwadhibiti maana yake hatutakuwa na pamba na itakuwa kazi bure" amesema Mwanri.

Aidha amesema zao la pamba kwa sasa limevamiwa na wadudu wa aina nne ambao ni kidung'ata, chawa jani, kanga mbili na funza.

Akizungumzia jitihada zilizochukuliwa na bodi ya pamba ili kukabiliana na wadudu hao mkaguzi wa pamba wilaya ya Bariadi Thadeo Mihayo amesema tayari wamepokea ekapack 548 za viuatilifu kwa ajili ya kukabiliana na wadudu hao.

"Pamba ilipofikia saizi ni hatua moja mhimu sana ya kuzuia wadudu tukishindwa hapa tunaharibu juhudi zote tulizo anza nazo tangu awali" amesema Mihayo.

Issa Mteve ni afisa kilimo wilaya ya Bariadi ameeleza kuwa tangu kuanza kwa kampeni ya kuhamasisha kilimo cha zao la pamba chenye tija nchini katika halmashauri ya mji wa Bariadi asilimia 80 ya wakulima wanalima kwa kufuata kanuni kumi za kilimo cha pamba.

" Wakulima wamehamasika wanalima kwa msitari na tunaendelea kuwapa elimu ili kupata uelewa zaidi wa kilimo sahihi chabpamba," amesema Mteve.


Aidha baadhi ya wakulima wa zao hilo wameainisha kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa pampu za kupulizia viuatilifu ambapo wameiomba bodi ya pamba nchini kusaidia kumaliza changamoto hiyo.


"Pampu moja inatumiwa kwa awamu na wakulima zaidi ya watano, mtu akiwa na ekari nyingi ni changamoto kumaliza kupiga dawa kwa sababu ni lazima awape wengine watumie hali inayo sababisha kushindwa kupiga dawa kwa wakati" amesema Charles Masunga mkulima wa mtaa wa Sanungu Bariadi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments