Post Top Ad
Sunday, March 20, 2022
SIMBA SC YACHAPWA 3 - 0 IKICHEZA NA ASEC MIMOSES
*************
NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Simba imeshindwa kutamba kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kupokea kichapo mabao 3-0 dhidi ya ASEC Mimoses .
Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya aina yake ambapo licha ushindi walioupata ASEC Mimoses kipa wa Simba Sc Aishi Manula ameweza kuokoa hatari nyingi ikiwemo penati mbili katika kipindi cha kwanza na cha pili.
Mabao ya ASEC Mimoses yamewekwa kimyani na mshambuliaji Stephene Aziz Ki, Aubin Kramo pamoja na lingine likifungwa na Karim Konate.
Simba Sc itasubiri mechi yake ya mwisho wakiwakaribisha US Gendermerie mchezo ambao utachezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Malunde 1 blog ni blog ya Kiswahili maarufu duniani kwa habari za Matukio, Siasa, Magazeti, Nyimbo za asili na habari za kusisimua.
No comments:
Post a Comment