NEMC YAKUTANA NA WATAALAM WA MAZINGIRA MAONESHO YA DOHA QATAR

Wageni wakiuliza maswali yanayohusiana na utunzaji na uhifadhi wa Mazingira.
Picha ya pamoja Kati ya wawakilishi wa NEMC pamoja na wawakilishi wa Kampuni ya ORKA Trading inayopatikana nchini Qatar inayojishughulisha na utengeneza na uuzaji wa sensors mbalimbali kwa ajili ya kutambua uchafu na ubora katika mazingira.Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya ORKA bw.Mohamed Abdalka akifafanua jinsi mashine zake za kubaini uchafuzi wa Mazingira jinsi zinavyofanya kazi.

Akionesha vifaa vya kisasa vinavyopima kwa haraka na kutoa majibu sahihi ya uchafuzi wa Mazingira.
Mteja aliyetembelea Banda la NEMC ambaye anaishi Dubai akisaini namba maalum kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali kuhusu NEMCElimu na fursa zilizopo nchini Tanzania kupitia Sekta ya Mazingira zikifafanuliwa kwa wateja waliotembea banda la NEMC.

**********************

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwenye Maonesho ya Kilimo na Mazingira 9 Agriteq & Enviroteq) Doha-Qatar wameendelea kutoa elimu na kutafuta wawekezaji na tekinologia katika masuala yahusuyo utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

Leo tarehe 12/03/2022 washiriki wa NEMC wamepata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Kampuni ORKA Trading W.L.L hapa nchini Qatar inayojishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa sensors (Vihisi) mbalimbali kwa ajili ya kutambua uchafuzi na ubora katika mazingira kama vile kwenye udongo, hewa, taka hatarishi, mimea, maji, viwandani, mikusanyiko, nyumbani na mashuleni.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ORKA Trading W.L.L. Bw. Mohamed Abdalla amelieleza Baraza kuwa utunzaji wa mazingira ni suala muhimu sana kwa maendeleo ya Nchi husika hivyo utambuzi wa vihatarishi vyovyote katika mazingira unafanikiwa kwa kutumia teknologia za kisasa zinazorahisisha utoaji wa majibu sahihi kwa muda mfupi ili kusaidia kufanya maamuzi sahihi ili kuokoa mifumo ikolojia isiharibiwe.

Bw. Mohamed Abdalla ameahidi kushirikiana na NEMC kama msimamizi mkuu wa Mazingira Nchini kwa kutoa tekinolojia, vifaa (Potable monitoring tools) vya kisasa na ujuzi wa namna ya kutumia ili kurahisisha utendaji kazi wa Baraza na za wateja wake (wawekezaji Nchini Tanzania) katika utunzaji wa mazingira kupitia matumizi ya vihisi vya uchafuzi wa mazingira.

Naye Meneja wa Kanda ya Ziwa Viktoria, anayeshiriki katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo na Mazingira Bw. Jarome Kayombo amesema uhusiano wa kitaaluma na kitechnolojia kati ya NEMC na Kampuni ya ORKA Trading inayojishughulisha na utengenezaji na uuzaji wa Potable monitoring tools ( sensors) ni wa mhimu kwa Baraza hususani katika Kurugenzi ya Uzingatiaji na Utekelezaji wa sheria (DECE) na Kurugenzi ya Utafiti na Usimamizi wa Mazingira (DERM) kwa lengo la kutambua uchafuzi wa mazingira na kuweza kutoa majibu ya kisayansi kwa wakati. 

Hivyo mahusiano haya ni mhimu kuyaendeleza kwa faida ya pande zote mbili na pia itakuwa ni mkombozi mkubwa sana kwa nchi yetu hasa katika kipindi hiki ambapo kama nchi tunashuhudia uwekezaji mkubwa katika Nyanja zote za kiuchumi, kijamii na kimazingira.

 Pia kama nchi ni wakati sahihi wa kutunza mazingira kwa kutumia technolojia za kisasa ili kuweza kuwafikia wadau wengi na kwa muda mfupi.

“Aidha, maonesho haya yamekuwa fursa muhimu kwa Baraza kuweza kukutana na wadau mbalimbali na kubadilishana ujuzi, uzoefu na tekinolojia na hivyo kampuni ya ORKA Trading wamevutiwa na kuahidi kushirikiana na NEMC kwa ajili ya kubadilishana technolojia na kusambaza vifaa vya kisasa vya kutambua aina mbalimbali za uchafuzi ili kusaidia juhudi za serikali kutunza mazingira yetu kwa ajili ya uhai wetu na viumbe hai” alisema Bw. Kayombo.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments