MFALME ZUMARIDI NA WENZAKE 84 WAFIKISHWA MAHAKAMANI


Diana Bundala maarufu kama ‘Mfalme Zumaridi’ na wenzake 84 leo Alhamisi Machi 17, 2022 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza kusomewa maelezo ya awali katika mashtaka matatu ikiwamo usafirishaji haramu wa binadamu.

Makosa mengine ni pamoja na kusanyiko lisilo na kibali na kuzuia maofisa wa Serikali kutimiza wajibu wao.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo saa 6:00 mchana mbele ya ya Hakimu mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Monica Ndyekubora.

Huyu ndiyo ‘Mfalme Zumaridi’

Kwa miaka kadhaa sasa, ‘Mfalme Zumaridi’ ambaye jina lake halisi ni Diana Bundala, ni miongoni mwa wahubiri wa dini wanaovuma ndani na nje ya Jiji la Mwanza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post