POLISI KAGERA WAMKAMATA JAMAA AKIWA NA FUNGUO BANDIA 97 ZIMO 'MASTER KEYS'

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera ACP Wankyo Nyegisa akionesha funguo zilizokamatwa
Baadhi ya funguo bandia zilizokamatwa

Na Mbuke Shilagi - Kagera

Jeshi la polisi mkoani Kagera linamshikilia mwanaume aliyefahamika kwa jina la Furaha Hansy mwenye umri wa miaka 58 mkazi wa mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kukutwa na funguo bandia 97, zikiwamo funguo nne (master keys) ambazo zinaweza kufungua mlango wowote. 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera ACP Wankyo Nyegisa amesema kuwa alikamatwa Machi 07, 2022 katika nyumba moja ya kulala wageni iliyoko wilayani Muleba.

Kamanda huyo amesema kuwa baada ya kukamatwa alihojiwa na kukiri kutumia funguo hizo katika matukio mbalimbali ya uvunjaji  wa maduka na nyumba za watu katika mikoa ya Dar-es- Salaam, Mbeya na Kagera.

Aidha jeshi la polisi limekuwa na opareshen mwendelezo tangu Machi 1 mpaka 9 mwa huu na kukamata watuhumiwa 39 kwa tuhuma mbalimbali katika wilaya tofauti mkoani humo.

Ameongeza kuwa kati ya watuhumiwa 39 watuhumiwa watano wanashikiliwa kwa tuhuma za kupatikana na pombe haramu ya moshi (gongo) lita 20, watuhumiwa tisa wakikamatwa kwa tuhuza za mauaji, mtuhumiwa mmoja kwa kwa tuhuma za wizi wa ng'ombe 20 na mwingine mmoja kwa tuhuma za wizi wa pikipiki.

Sambamba na hayo amewataka wananchi wote kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa za uhalifu ili kuepusha na kutokomeza vitendo vya mauaji mbalimbali huku akitoa onyo kali kwa wale wote wanaojihusisha na vitendo viovu kuacha mara moja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post