FREEMAN MBOWE AKUTANA NA RAILA ODINGA


Mwenyekiti wa Chadema Freeman Aikaeli Mbowe jana amekutana na Mheshimiwa Raila Amolo Odinga, Mgombea Urais wa Muungano wa Azimio la Umoja na Mheshimiwa Martha Karua, Kiongozi wa Chama cha NARC Kenya Jijini Nairobi.

Kupitia kwao, Mheshimiwa Mbowe amewataka Wakenya wote kushikamana kuhakikisha kuwa uchaguzi wao unakuwa wa haki, huru na wazi.

Kipekee, amewasihi Viongozi na Wagombea hao kuhakikisha vurugu za uchaguzi zilizotokea nchini Kenya miaka ya nyuma na kusababisha vifo vya Wakenya kamwe havijirudii tena.

Aidha, amewataka kutambua nafasi ya Taifa la Kenya katika kuendeleza Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu katika Eneo la Jumuia ya Afrika Mashariki na kwamba wanapaswa wakati wote kulinda na kuendeleza mafanikio hayo.

Mheshimiwa Mbowe amewatakia Wakenya wote mchakato mwema wa Uchaguzi wao wa August 2022.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post