VYUO VYA UDEREVA MATATANI JINAMIZI LA AJALI TANZANIA

 Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Hamad Masauni akiongea kwenye kikao chake na baraza la taifa la usalama barabarani Ofisini kwake leo Mtumba Jijini Dodoma.


Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 Blog-DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya mambo ya ndani imesema kuna haja ya kupitia upya mfumo mzima wa utoaji mafunzo na leseni kwa madereva katika Vyuo vyote nchini ili kubaini kama vinakidhi mahitaji hali .


Hatua hii imekuja wakati ambao matukio ya ajali za barabarani yanazidi kuongezeka siku hadi siku na kukatisha uhai wa watu wengi jambo ambalo serikali imesema linapoteza nguvu kazi ya taifa hivyo linapaswa kutiliwa mkazo zaidi hali itakayo punguza ajali zote zisizo za lazima.


Hayo yamezungumzwa leo jijini Dodoma na  Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi  Hamad Masauni katika kikao chake na baraza la taifa la Usalama barabarani ambapo alisema  ikiwa agizo hilo litazingatiwa na kufanywa kwa weledi litadhibiti mfululuzo wa matukio ya ajali ambazo zimekuwa zikitokea.


"Nafikiria Kuna haja ya jeshi  la polisi likague vyuo vote vinavyotoa leseni za udereva ili kubaini kama vinakidhi mahitaji tuliyonayo ili madereva wanaomaliza wawewanatambua dhamana ya kazi yao,"amesema


Aidha ametoa miezi sita kwa wamiliki wa maroli na mabasi waliotoa vidhibiti mwendo kuvirejesha katika magari hayo  huku ikitangaza operesheni kali ya usalama barabarani  na hatua kali kwa watakao kaidi.


Amesema kutokana  na utafiti uliofanywa na Chuo Kukuu cha Dar es Salaam(UDSM) kwa miaka kadhaa iliyopita  ilionyesha kuwa asilimia 76 ya ajali zote husababishwa na vyanzo vya binadamu ikiwemo uzembe, jambo jingine ni ubovu wa magari ambapo huchangia kwa asilimia nane huku ubovu wa miundombinu ukichangia kwa asilimia 16.

"Maelekezo ambayo ntayatoa leo hapa ni kupata suruhisho la ajali hapa nchi na kwa kuanza nataka mabasi na maroli  yawe na vidhibiti mwendo na ndiyo sheria inavyotaka lakini tumeshuhudia baadhi ya wamiliki wa magari wanapoingiza vyombo vyao wamekuwa wakitoa,"amesema.


Waziri Masauni amesema dhamira ya wanaotoa vifaa hivyo  ni kutaka kuvunja sheria kwa sababu vifaa hivyo vimewekwa kwa lengo la kudhibiti mwendo ili gari lisitembee kwa mwendo usiozidi kilometa 80 kwa  saa.


"Hii ni sheria ambayo ipo na tunataka sasa hivi sheria hii isimamiwe kwahiyo maelekezo yangu kwa jeshi la polisi ni kusimamia sheria hii na kwa wamiliki wa magari ambao watakiuka sheria hii hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao na kwa wale ambao wanatarajia kuingiza mabasi yao au maroli waachane kabisa na na mawazo ya kutoa speed  Govornor  na kwa wale waliotoa tunatoa muda wa miezi sita wawe wamerejesha vifaa hivyo,"amesema.


Katika hatua nyingine Waziri masauni ametaja chanzo cha ajali iliyotokea Morogoro na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 22 alisema  kama lingekuwa na ubora lisingeweza kusababisha vifo vya watu wengi kama ilivyotokea.


"Ile gari ilikuwa imefungwa vifaa ambavyo hutumika kuweka zege katika nyumba hivyo ndiyo vilikata viungo vya watanzania wenzetu  na hapa natoa maelekezo kufanya uchunguzi ili kubaini kiwanda kilichotumika kutengeneza gari hiyo na kufanya msako nchi nzima kwa kiwanda kinachofanya vitu vya ovyo kuwakamata na kuwachukulia hatua,"amesema


Ameongeza kuwa:"Hatuwezi kucheza na maisha ya watanzania hatuwezi kukubali kupoteza maisha ya watu wengi kwasababu ya malsai au uzembe wa watu wachache  na serikali imeweka fedha nyingi katika mifumo halafu watu wengine wanachezea hili jambo halikubaliki,amesema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments