GYPSON APONGEZA KASI YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA BUKOBA

Meya wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Mhe. Godson Gypson

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Mtahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Mhe. Godson Gypson amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa maendeleo anayoyatenda katika Manispaa yake tangu aliposhika nafasi yake ya Urais baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.


Amesema hayo leo Machi 17,2022 ofisini kwake akizungumza na Malunde 1 blog katika Kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.


Amesema miradi mbalimbali imeendelea kutekelezwa ndani ya manispaa ya Bukoba ikiwemo madarasa 30 yaliyogharimu takribani shilingi milion 600, ujenzi wa ujenzi wa zahanati kwa kila kata, ujenzi wa hospitali ya wilaya unaoendelea hivi sasa ambao umefikia asilimia 75 na miradi mingine mbalimbali ya kimaendeleo.


Pia amelipongeza Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Bukoba kwa kuendelea na umoja wao katika kuendeleza maendeleo na kumuunga mkono Rais Samia pamoja na viongozi wote wakiongozwa na mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge.


Aidha ameiomba serikali kuwajengea kituo cha mabasi ambacho kitakuwa chenye ubora pamoja na soko kuu la Bukoba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post