
Mke wa mzee Mrema anayejulikana kwa jina la Doreen Kimbi amesema kuwa atamrudisha mzee Mrema ujanani.
"Mpaka kufikia hivi alivyo nimemfanya hivi. Katika kipindi cha uchumba nimemweka kuwa sawa, vitu vyote anavyohitaji anavipata. Kwa sasa amebadilika, nimeamua mwenyewe na sijashurutishwa na mtu na watarajie kuona anapendeza, nataka hadi awe kijana", amesema Doreen.
"Mimi si mwanamke wa kupewa, nimesimama mwenyewe na hata mali ninazo. Nilianza kujitafutia mimi, siendi kwake (Augustino Mrema) kutafuta mali. Lakini nikimlea vizuri akanipa mali si vibaya kwani ni mke wake",amesema Doreen




Social Plugin