Picha : RC MJEMA AONGOZA KIKAO CHA WADAU KUJADILI MAENDELEO YA ELIMU SHINYANGA...ASISITIZA ELIMU NI BURE

 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akifungua kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Machi 3,2022 chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga. 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria walimu watakaobainika kudai malipo kwa wanafunzi akisema elimu ni bure.

Mjema ametoa agizo hilo  leo Alhamisi Machi 3,2022 akifungua kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

“Kumekuwa na upotoshaji huko mtaani kuwa wazazi wanatakiwa kulipa ada. Napenda kusisitiza kuwa elimu ni bure,hakuna malipo, mwalimu yeyote atakayebainika kuchangisha fedha achukuliwe hatua. Tutaendelea kutatua changamoto zilizopo ikiwemo utoro,chakula, upungufu wa walimu,nyumba za walimu n.k”,amesema Mjema.

“Tunachokwenda kufanya sasa ni kuboresha mazingira yaliyopo shuleni. Wote tunatakiwa tushikamane, upande wa shule binafsi na za serikali. Tunataka shule zetu ziingie kumi bora kitaifa kila mwaka.Walimu na wadau wote tuwe wabunifu, wakurugenzi tuwe na ubunifu pia kwa kuwapa motisha walimu ikiwemo kuwapatia nyumba, mtaona hawataondoka, hawatakimbia na ufaulu utaongezeka.

Waheshimiwa Ma DC (Wakuu wa wilaya) nendeni mkasimamie upatikanaji wa chakula shuleni, Tunataka lishe bora shuleni ili watoto wakue vizuri. Tukasimamie pia mdondoko, watoto wafuatiliwe wako wapi, watoto wanatakiwa wawe shule kama tulivyowaandikisha, tusikubali kuwa chini ya asilimia 100”, amesema Mjema.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akifungua kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Machi 3,2022 chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akifungua kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Machi 3,2022 chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akifungua kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Machi 3,2022 chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.
Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zuwena Omary akizungumza kwenye kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Machi 3,2022 chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.

Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Dafroza Ndalichako akizungumza kwenye kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Machi 3,2022 chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa (kushoto) na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko wakisoma nyaraka kwenye kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Machi 3,2022 chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kwenye kikao cha Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga leo Alhamisi Machi 3,2022 chenye lengo la kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.
Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.
Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.
Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.
Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.

Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga.
Wadau wa elimu Mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya elimu ili kuboresha elimu mkoani Shinyanga. 

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Soma pia

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments