WANAWAKE BODI YA MAJI BONDE LA MAJI ZIWA VICTORIA WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUSAIDIA WAZEE BUKUMBI

WANAWAKE  kutoka Bodi ya maji bonde la Ziwa Victoria wamefika katika kituo cha kulea Wazee cha Bukumbi mkoani Mwanza na kutoa mahitaji mbalimbali yakiwemo mavazi na chakula,ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani inayofanyika tarehe 8 ya mwezi Machi kila mwaka.

kituo hicho cha kulea wazee wasiojiweza kinachomilikiwa na serikali kina jumla ya wazee 31 kati yao wanaume ni 9 na wanawake ni 21 na mtoto mmoja.

Akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali,Afisa uhusianao wa bodi hiyo Perpetua Massaga.

"Sisi kama wanawake  tunatambua mchango wa wazee hawa  katika jamiii yetu hivyo hatuwezi kuwasahau  ni lazima tuwakumbuke na ndo maana tumekuja kuwaletea zawadi hii kidogo", alisema Massaga.

Kaimu mkuu wa kituo hicho cha kulea wazee, Josephine Simba amewashukuru wanawake hao Kwa kuwakumbuka wazee na kwamba kwa sasa kituo hicho kinakabiliwa na changamoto ya uzio ili kuimarisha ulinzi kwa wazee.

"Tunaishukuru sana serikali ya awamu ya sita inawakumbuka wazee wetu imeboresha huduma ya afya Kwa wazee hawa na kwa Sasa wazee wote katika kituo hiki wanakadi za Bima ya afya",alisema Simba.

Baadhi ya wazee katika kituo hicho wakiwemo, Mariam Ally  amewashukuru wanawake hao wa bodi ya maji kwa kuwaletea zawadi na kuomba watu wengine wawakumbuke kwenda kuwasalimu na kuwapelekea mahitaji mengine.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments