KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA SERIKALI NA AUWSA KWA USIMAMIZI MZURI WA MRADI MKUBWA


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA) Mhandisi Justine Rujomba akitoa maelezo kwa kamati ya bunge ya kudumu ya uwekezaji na mitaji ya umma katika mradi wa maji Chekereni.

Na Rose Jackson, Arusha

Kamati ya kudumu ya bunge uwekezaji wa mitaji ya umma imepongeza serikali,bodi na menejiment ya uongozi wa  AUWSA kwa usimamizi wa mradi mkubwa wa maji wa shilingi bilioni 520.


Akizungumza katika ziara iliyofanywa na kamati hiyo ya kutembelea na kukagua mradi wa AUWSA wa mabwawa 18 ya kutibu maji mwenyekiti wa kamati hiyo ambae ni mbunge wa Ilala Jerry Slaa ameipongeza serikali na bodi ya  AUWSA kwa kuwa kazi hiyo imefanyika kwa asilimia 82.

Ameipongeza serikali pamoja na menejimenti na uongozi kwa kusimamia mradi huo kwa uadilifu mkubwa kwani kazi ni nzuri na umeshakwishafikia asilimia 82 ya utekelezaji na matunda yake yameshaanza kuonekana.

"Kwa niaba ya wabunge wenzangu na nikiwa mwenyekiti wa kamati hii niipongeze serikali ya Samia Suluhu Hasan pamoja na menejiment ya AUWSA kwa usimamizi nzuri mlioufanya kiuadilifu mnaonyesha namna ambavyo mmesimamia vema mradi huu mkubwa", aliongeza Slaa

Amewataka wananchi wa Arusha kutunza miundo mbinu hiyo ili kuweza kuleta tija kwa serikali kwa ajili ya kuboresha uchumi wa nchi.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa AUWSA mhandisi Justine Rujomba amesema kuwa anashukuru kwa kamati hiyo kukagua miradi yao na kazi yao Ni kuhakikisha wanatimiza malengo ya mradi huo.

Naye mwenyekiti wa bodi ya AUWSA mhandisi Richard Masika ameeleza kuwa Hadi Sasa Utekelezaji umefikia asilimia 82 na wananchi wameshaanza kuona manufaa yake na kwa sasa wapo hatua ya pili ya mradi.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments