WAZIRI NAPE NNAUYE AFANYA UTEUZI WAJUMBE BODI YA KAMPUNI YA MAGAZETI YA SERIKALI (TSN)


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amefanya uteuzi wa Wajumbe sita wa Bodi ya Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 2 Februari, 2022 kama ifuatavyo:-

1. Bw. Titus Modestus Kaguo – Meneja wa Uhusiano kwa Umma, Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji (EWURA);
2. Bw. Erasmus Masumbuko Uisso – Mkurugenzi Msaidizi, Mipango na Bajeti, Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam;
3. Bi. Teddy Donacian Njau – Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, \Nizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari;
4. Bw. Habibu Juma Suluo – Mkurugenzi wa Fedha, Rasilimaliwatu, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Dar es Salaam;
5. Dkt. Julius Mutabaazi Lugaziya – Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala Tanzania, Dar es Salaam: na
6. Bw. Andrew Lubella Gewe – Meneja, Kampuni ya Ujenzi na Ushauri katika Masuala ya Ujenzi ya “Africa Consulting Limited” Mpanda, Katavi.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments