WADAU WA SANAA WAMPONGEZA WAZIRI MCHENGERWA KWA UBUNIFU


**************

Na John Mapepele

Wadau wa Sanaa Wadau wa Sekta za Sanaa wamempongeza Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa kwa ubunifu wake wa kuanzisha mfumo wa kuongea na wadau moja kwa moja wakati wowote, usiku na mchana huku wakisema hatua hiyo inatasaidia kuleta mageuzi makubwa na ya haraka katika tasnia hiyo.

Akizungumza majira ya saa tatu usiku, Februari 3, 2022 jijini Dodoma baada ya kujadiliana mambo mbalimbali ya uzalishaji wa filamu na program za redio na televisheni Mkurugenzi wa Kampuni ya Authentic Media ya jijini Dar es Salaam, Maximilian Rioba amesema ukaribu unaujengwa sasa baina ya Wizara na wadau utaleta mafanikio makubwa kwa wasanii.

"Kikubwa nimefarijika kuona kwamba hata usiku kama huu milango imefunguka nimeweza kuonana na Mheshimiwa Waziri na kujadili masuala ya maendeleo ya tasnia yetu" amefafanua Rioba

Amesema kitendo cha Mhe. Waziri kinawatia moyo wazalishaji wa kazi za Sanaa na kinapeleka salamu kwa wadau wengine kuwa Serikali inafanya mapinduzi makubwa katika Sekta ya Sanaa.Hivyo jambo la maana kwa sasa ni kwa wasanii kuweza kuzalisha kazi zenye ubora ili kuweza pia kuuza katika masoko ya kimataifa na kuitangaza Tanzania.

Kwa upande wake Mhe. Mchengerwa amesema amepata mambo mengi baada ya kumsikiliza ambapo amefafanua kuwa anakwenda kuwasikiliza wadau wote katika kikao cha wadau wote kitakachofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Amesema anaamini endapo uwekezaji mzuri utafanyika kwenye uzalishaji wa kazi za ujumla kuna uwezekano wa kuuza kazi hizo kwenye Netflix na kujipatia kipato chao na taifa kwa ujumla.

Amesema anatambua kuna baadhi ya wasanii waafrika walishawahi kutengeneza kazi zao na kujipatia fedha nyingi, hivyo mwelekeo wa Serikali ni huo wakuona vijana wanafaika na kazi hizo.

"Tunataka kila kijana wa kitanzania atambue kuwa eneo la kukimbilia ni kwenye Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo" ameongeza

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post