JESHI LA POLISI NCHINI LATAKIWA KUWEKEZA KWENYE TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO KUZUIA UHALIFU


Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew akifungua mafunzo ya makosa ya mtandao kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka wa Jeshi la Polisi Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa Zimamoto leo Jijini Dodoma. Picha na Alex Sonna

Na Dotto Kwilasa-Malunde 1 Blog- DODOMA.

NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Andrew Kundo amelitaka jeshi la polisi nchini kuwekeza kwenye Teknlojia ya mawasiliano ili kupambana na uhalifu wa mtandaoni.

Hayo yamesemwa leo  jijini hapa na Naibu Waziri huyo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya usalama mtandaoni kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka na kueleza kuwa hali hiyo itarahisisha utendaji kazi wa Jeshi hilo.

"Ikiwa mtaamua kuwekeza kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka wataona umuhimu wa Teknlojia na kuweza kurahisisha utendaji kazi na kuweza kupambana na uhalifu wa mtandao kwa njia sahihi ,"amesema.

Pamoja na hayo amelitaka jeshi hilo kuona haja ya kuongeza ujuzi wa namna ya kukabiliana na uhalifu wa mtandaoni ili kuwa na Jeshi la kisasa linalojibu kiu ya watanzania katika utekelezaji wa huduma bora.

Kwa upande wake Kamishna msaidizi mwandamizi  wa polisi(SACP)Deusdedit Nsimeki,amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa yatawasaidia kupata uelewa wa masuala ya mtandao kwa kuhusisha  makosa ya mtandao.

Akizungumza  kwa niaba ya Mkurugenzi wa mashtaka nchini (DCI),Nsimeki amesema kupitia mafunzo hayo itasaidia polisi wengi kuondoa dhana chafu ya kugeuza taaluma hiyo kama sehemu ya kujipatia kipato.

"Mafunzo haya ni muhimu sana kwa wakati huu, yanatujenga  kumsaidia mwananchi sio kujipatia kipato, kumekuwa na malalamiko toka kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa na kesi ya kupotelewa na simu zao kulipia gharama kubwa tofauti na simu ambayo imepotea na hivyo kuharibu taswira ya jeshi na taaluma kwa ujumla,"amesema na kuongeza;

Mafunzo hayo yatasaidia kuongeza tija na uadilifu katika utendaji kazi  ikiwa ni pamoja na kupambana na uhalifu na kusaidia kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa,"amesema. 


Naye Kamishna wa Polisi -Uchunguzi wa kisayansi (CP)Shabani Hiki,amesema ni wajibu wa kila polisi kuhakikisha anafanya kazi vizuri na kuhakikisha kila raia anakuwa salama ili kuongeza uaminifu na taswira nzuri.


"Ni wajibu wetu kufanya kazi kwa bidii hilo ndilo jukumu letu,tukifanya kazi kwa uaminifu na kushughulikia kero za kimtandao  itasaidia kupunguza malalamiko ya wananchi kwa kuwa tutakuwa tunawatendea haki kama kazi yetu inavyotuagiza kufanya,"amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments