BENKI TCB YAKABIDHI HUNDI YA MKONO WA POLE KWA FAMILIA ZA WAANDISHI WA HABARI WALIOFARIKI KWENYE AJALI


Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mh Amina Makilagi (wapili kulia) akikabidhi hundi kwa ndugu wa Marehemu waandishi wa habari waliopoteza maisha Januari 11,2022

Na Hellen Mtereko, Mwanza
Benki ya Biashara ya Tanzania (Tanzania Commercial Bank- TCB PLC) imekabidhi hundi ya Shilingi Milion 15 ya mkono wa pole kwa familia za waandishi wa habari waliopoteza maisha kwenye ajali ya gari wakielekea ziarani Ukerewe.


Hafla hiyo ya kukabidhi hundi imefanyika leo Jumatatu Februari 21,2022 katika ukumbi wa Mwanza Hotel Jijini Mwanza.


Benki ya TCB imekabidhi hundi kwa familia za waandishi hao ambao ni Anthony Chuwa, Johari Shani na Husna Mlanzi kwa sababu enzi za uhai wao walikuwa wanachama wa Wanahabari Bima Group kutokana na kifurushi kinachotolewa cha Alliance Life Assurance kwenye Benki hiyo.

Akikabidhi hundi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi amewapongeza baadhi ya waandishi wa habari waliokwisha kujiunga na Wanahabari Bima Group huku akiwataka ambao bado hawajajiunga wajiunge ili waweze kupata msaada pindi majanga yanapowakumba.


Amesema kuwa kitendo cha waandishi wa habari kuamua kujinyima na kuanza kuwekeza kwenye Benki hiyo ni kitendo cha uzalendo ambacho leo kimeweza kuwafuta machozi familia za marehemu.

Makilagi amewaasa waandishi ambao tayari wamekwisha kujiunga na bima hiyo kuwa waendelee kushirikiana na kupendana ili umoja huo uzidi kuimarika na kuwa chachu kwa wengine.

Makilagi ametoa ushauri kwa Benki hiyo kuanzisha vifurushi vingine vipya vya kuwasaidia waandishi kikiwemo cha ada ili mwanachama anaposhindwa kumlipia ada mtoto Benki iweze kumsaidia kutokana na kile alichowekeza.


Kwaupande wake Mkuu wa kitengo cha bima kutoka Tanzania Commercial Bank (TCB), Francis Kaaya amesema kuwa wamefanikiwa kutoa hundi hiyo kwa kushirikiana na alliance life assurance ambao wamekuwa wakilipa mafao hayo kwa wakati.

Naye Afisa Mauzo na Masoko kutoka Alliance Life Assurance, Jawa Masomo amesema kuwa wamekuwa wakilipa mafao kwa wakati ili yaweze kuwasaidia wafiwa katika kutatua shida za hapa na pale.


Akizungumza kwa niaba ya wafiwa ambao walikuwepo katika makabidhiano ya hundi bw, Chuwa amesema kuwa wamefarijika sana kutokana na umoja huo walioanzisha wanahabari kwani ni kitu ambacho kimetupa faraja sana mioyoni mwetu kutokana na kwamba Marehemu hao wameacha Watoto, wajane hivyo fedha hizo zitakwenda kuwasaidia.
Mkuu wa kitengo cha bima kutoka Tanzania Commercial Bank (TCB), Francis Kaaya akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi ya sh. Million 15 kwa familia za Marehemu
Waandishi wa habari, viongozi wa dini na ndugu wa Marehemu wakiwa katika maombi ya kuwaombea marehemu leo hii katika hafla ya kukabidhi hundi
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mh Amina Makilagi akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi hundi kwa ndugu wa Marehemu waandishi wa habari waliopoteza maisha januari 11,2021
Waandishi wa habari na ndugu wa Marehemu waliohudhuria kwenye hafla fupi ya kukabidhi hundi

Soma pia : 

GARI LA WAANDISHI WA HABARI LAGONGANA NA HIACE...WATU 14 WAFARIKI, WAMO WAANDISHI


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments