" SAGINI AITAKA SEKRETARIETI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI BINADAMU

SAGINI AITAKA SEKRETARIETI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI BINADAMU


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akizungumza na Watendaji wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu- ATS, leo Februari 11,2022 jijini Dodoma.


Katibu wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu- ATS, Separatus Fella akielezea utendaji kazi wa Sekretarieti hiyo mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini leo Februari 11,2022 jijini Dodoma.


Afisa wa Sekretariet ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu- ATS, Alex Lupilya akieleza changamoto zinazowakabili Sekretarieti hiyo wanapopambana na biashara haramu ya usafirishaji binadamu nchini kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini leo Februari 11,2022 jijini Dodoma.

..........................................................................

Na Mwandishi wetu,

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amewataka Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu kutumia Vyombo vya Habari kuelimisha Umma juu ya madhara ya kujihusisha na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu, Elimu ambayo itawasaidia kutojihusisha katika matukio hayo.

Naibu Waziri Sagini ameyasema hayo leo alipotembelea Ofisi za Sekretariti ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu zilizopo Kambarege Tower Jijini Dodoma ili kufahamu shughili wanazotekeleza.

Amesema uandaaji wa vipindi vya uelimishaji vitakavyorushwa katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Televisheni, Radio pamoja na mitandao ya kijamii itasaidia wananchi katika ngazi zote kuwa na uelewa juu ya madhara yanayoweza kutokea ama kuwapata kutokana na kujihusisha na biashara hiyo haramu.

“Ni vema mkaanda programu mbalimbali za televisheni na radio zitakazowaelimisha Watanzania juu ya Biashara haramu ya Usafirishaji binadamu ili waweze kujiepusha nazo huko mtaani”

Aidha Naibu Waziri Sagini ameitaka Sekretariet hiyo kutumia vyombo hivyo vya habari kuelimisha jamii hususani vijana kutumia fursa sahihi za ajira zilizopo nchini ili kupunguza vijana kurubunika kirahisi kwa kujiingiza kwenye vitendo vya biashara hiyo haramu kutokana tu na kutokuwa na uelewa wa madhara. Jambo ambalo ni kinyume cha Sheria na Taratibu za Nchi yetu.

“Ni vema vijana wakaelimishwa namna ya kutumia ujuzi unaopatikana kwenye vyuo mbalimbali vilivyoko nchini ikiwemo VETA ili kuweza kujiajiri badala ya kutafuta maisha kirahisi nje ya Nchi ambayo yanakwenda kuwadhalilisha, muhimu vijana watumie fursa sahihi za kujiajiri zilizopo nchini”. Amesema Sagini. Aidha amesisitiza kuwa kuna haja ya kuimarisha mifumo ya Sekretariet ya kuwafuatilia vijana, kuwabaini na kuwazuia kujiingiza kwenye biashara haramu ya usafirishaji binadamu kabla hawajarubunika.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments