MWALIMU AUAWA KWA KUPIGWA KITU KIZITO..MAPENZI YAHUSISHWA

Na mwandishi wetu,Mpwapwa.

MWALIMU wa shule ya Msingi Kisokwe, Wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma Albert Kaguli (43) amekutwa ameuawa na watu wasio julikana kwa kupigwa kichwani na kitu kinachosadikiwa kuwa kizito.


Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP)Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa kina kubaini aliyefanya uhalifu huo.


Aidha amesema  jeshi hilo pia linamtafuta mtu mmoja anaye julikana kwa jina la Shukuran Maselo Kwa uchunguzi zaidi kwa kushukiwa  kushiriki katika mauaji hayo ambayo chanzo chake inadaiwa kuwa  ni wivu wa mapenzi. 


Kutokana na tukio hilo Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Josephat Maganga amelaani kitendo hicho na kuwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkoni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments