MRISHO MPOTO ATEULIWA KUWA BALOZI WA MAJI NCHINI

Msanii wa muziki nchini Mrisho Mpoto
 

Na Mwandishi wetu, Malunde 1 Blog-MARA.


WAZIRI wa Maji nchini Jumaa Aweso amemteua msanii wa mziki Mrisho Mpoto kuwa balozi  wa Sekta ya maji ambapo atakuwa akihamashisha jamii kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa maji.


Hatua hiyo imekuja mara baada ya msanii huyo kuimba wimbo wenye maudhui yaliyosheheni takwimu sahihi za maji Katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi Katika mradi wa maji wa Bunda mkoani Mara.


Aidha hafla hiyo imeongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.


Akiongea kwenye hafla hiyo,Aweso amesema watanzania bado wanahitaji kuelimishwa kuhusu utunzaji wa vyanzo vya maji hivyo ni vema kuenzi Sekta hiyo kupitia sanaa.


"Nimemteua Mpoto kwa kuwa ni mahiri,atatumia sanaa yake kuitangaza sekta ya maji na rasilimali zake katika shughuli mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali,"amesema Aweso.


Mpoto ni mmoja kati ya wasanii bora wa muziki katika ukanda wa Afrika Mashariki aliyebobea katika kutumia vionjo vya kiasili kufikisha ujumbe kwa hadhira.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post