MTOA ROHO NJOMBE AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUUA MTOTO ALIYEKOJOA KITANDANI


Polisi Mkoani Njombe wanamshikilia Israel Msigwa maarufu kwa jina la Mtoa Roho (39) Mkazi wa Makambako kwa tuhuma za kumsababishia kifo Mtoto wake Haskad Msigwa (7) kwa kumuadhibu kwa nyaya za umeme na fimbo kwa sababu amekojoa kitandani.

RPC wa Njombe Hamis Issah amesema; “Huyu amemuadhibu Mtoto wake kwa kutumia nyaya za umeme pamoja na fimbo na matokeo yake amemsababishia kifo Mtoto wake alafu akakimbilia Kilosa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

“Mzazi huyu alitoweka na alipotoweka tumemkamata jana eneo la Kilosa Mufindi mjini Mafinga na sasa tunamshikilia lakini mtoto amepoteza maisha, tukikamisha upelelezi sheria zitafuata mkondo wake” amesema RPC Issah.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments