MALKIA WA UINGEREZA AKUTWA NA CORONA BAADA YA KUPIMWA


Malkia Elizabeth wa Uingereza amekutwa na maambukizi ya virusi vya corona . Kasri la Buckingham limesema, Malkia ana dalili za kawaida kama za mafua.

Malkia mwenye umri wa miaka 95, alikuwa akiwasiliana na mtoto wake mkubwa ambaye ndiye mrithi wake, Prince of Wales, ambaye alikutwa na virusi vya Corona wiki iliyopita.

Inaeleweka kuwa watu kadhaa wamepima virusi katika Windsor Castle, ambako Malkia anakaa.

Kasri la Buckingham limesema kwamba kiongozi huyo ataendelea kufanya shughuli zake nyepesi katika Kasri la Windsor katika kipindi cha wiki chache zijazo na ataendelea kutibiwa na kufuata miongozo yote ya kupambana na maambukizi vya virusi vya Corona.

Malkia Elizabeth tayari amepata chanjo tatu dhidi ya COVID. Malkia alipokea chanjo yake ya kwanza ya Covid mnamo 9 Januari 2021.

Hao yanajiri wakati serikal ya Waziri  Mkuu Boris Johnson, wiki ijayo itaondoa vizuizi vyote vilivyosalia vya kupambana na maambukizi katika mkakati wake wa "kuishi na virusi vya Corona" .


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post