KIKAO CHA SEKRETARIET YA SJMT NA SMZ CHAFANYIKA ZANZIBAR
Thursday, February 17, 2022
Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Bw. Thabit Idarous Faina akiongoza Kikao cha Sekretarieti ya Kamati ya Pamoja cha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ya kushughulikia masuala ya Muungano kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Vuga, Zanzibar leo tarehe 17/02/2022. Kushoto ni Mwenyekiti Mwenza wa Kikao hicho Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Ngelela Maganga. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Muungano Bw. Sigsbert R. Kavishe na Bi. Siajabu Pandu Mkurugenzi wa Uratibu wa Shughuli za Serikali katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais. wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia mjadala katika Kikao cha Sekretarieti ya Kamati ya Pamoja ya SJMT na SMZ ya kushughulikia masuala ya Muungano kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Vuga, Zanzibar leo tarehe 17/02/2022. Sehemu ya wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakifuatilia mjadala katika Kikao cha Sekretarieti ya Kamati ya Pamoja SJMT na SMZ ya kushughulikia masuala ya Muungano kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Vuga, Zanzibar leo tarehe 17/02/2022. Kulia ni Bw. Mussa H. Ali, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu na Bw. Seif Sh. Mwinyi Katibu Mkuu Wizara ya Nchi, Afisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala bora.Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Thabit Idarous Faina (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Ngelela Maganga na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) mara baada ya kukamilika kwa kikao cha Sekretariet ya Kamati ya Pamoja SJMT na SMZ ya kushughulikia masuala ya Muungano kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Vuga, Zanzibar leo tarehe 17/02/2022.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin