KIJANA AMUUA MAMA YAKE KWA MPINI WA JEMBE AKIMDAI LAKI 3Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linamshikilia kijana Herman John kwa tuhuma za kumuua mama yake kwa kumpiga na mpini wa jembe baada ya kuhitilafiana kifamilia.

Akizungumza na wanahabari kuhusu matukio mbalimbali ya uhalifu yaliyotokea mkoani humo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP James Manyama amesema tukio hilo limetokea wilayani Kakonko mkoani humo.

“Selina William 63, mkulima na mkazi wa Kakonko aliuawa kwa kujeruhiwa na mwanaye aitwaye Herman John ambaye alikuwa anamdai kiasi cha fedha Tsh 300,000.

“Huu ulikuwa ni mgogoro wa kifamilia kijana baada ya kuhitilafiana na mama yake, alipomuomba pesa hizo hakupewa na mama yake, hivyo akajichukulia sheria mkononi na kumpiga na mpini wa jembe uliosababisha umauti wa mama huyo.

“Jeshi la Polisi tulimkamata mtuhumiwa na tunamshikilia kwa mahojiano na uchunguzi ili sharia ichukue mkondo wake,” amesema Kamanda Manyama.

Katika tukio jingine, Kamanda Manyama amesema jeshi hilo limekamata sialaha mbalimbali zilizokuwa zikitumiwa na majambazi, huku wakifanikiwa kuwaua majambazi watatu wenye sialaha kwa kuwapiga risasi huku askari mmoja akijeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni.

Aidha, Kamanda Manyama ameeleza kuwa Jeshi hilo linawashikilia watu watatu akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Kabulanzwili aliyefahamika kwa jina la Joseph Mbwebwe kwa kukutwa akimiliki bunduki aina ya gobole kinyume cha sharia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments