Picha : EWURA CCC YATOA MAFUNZO YA HUDUMA ZA NISHATI NA MAJI KWA WENYEVITI WA MITAA MANISPAA YA SHINYANGA

Katibu Mtendaji wa EWURA CCC Mhandisi Goodluck Mmari akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na EWURA CCC kuhusu haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za nishati na maji.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA Consumer Consultative Council - EWURA CCC) Mkoa wa Shinyanga limetoa mafunzo kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa Manispaa ya Shinyanga ili kujenga na kukuza uelewa na ufahamu kuhusu haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za nishati na maji sambamba na kuwezesha upatikanaji na utoaji wa taarifa juu ya miongozo, sera, kanuni na sheria zinazosimamia huduma za maji na nishati kwa mtumiaji na wananchi kwa ujumla.

Mafunzo hayo yaliyokutanisha wenyeviti wa mitaa na vitongoji kutoka kata 10 za Manispaa ya Shinyanga yamefanyika leo Ijumaa Februari 25,2022 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC), Mhandisi Goodluck Mmari.

Akizungumza katika semina hiyo, Katibu Mtendaji wa EWURA CCC Mhandisi Goodluck Mmari amesema mafunzo hayo yamekuwa na tija kubwa kwa wenyeviti wa mitaa na vitongoji kwani mada zilizotolewa na mjadala uliofanyika unagusa huduma za nishati na maji na unagusa maisha ya watu.

“Kwa kiasi kikubwa lengo la Programu hii ya mafunzo limefanikiwa,lengo la semina hii ilikuwa ni kutoa elimu na tumejifunza mambo mengi ikiwemo kujua EWURA CCC ni kitu gani,mambo na utaratibu wa kuwasilisha malalamiko kwa sababu unapokuwa na malalamiko kama hujui utaratibu wa kuwasilisha utabaki na kero yako. Kama hujui sheria,hujui haki zako huwezi jua namna ya kuzidai”,amesema Mhandisi Mmari.

“Huduma zinazozalishwa hazitoshelezi,maji hayatoshelezi hivyo kila tunachokipata tunatakiwa kukitumia vizuri hata kama una hela ya kulipia bili lakini kwanini umwage maji, kwanini utumie maji hovyo, unapotumia maji ujue kuwa kuna watu hawana hiyo huduma. Tutumie vizuri huduma ili huduma ziweze kuwafikia watu wengi zaidi ambao hawafaidiki na hizi huduma”,ameongeza Mhandisi Mmari.

Amewataka wenyeviti wa serikali za mitaa waliopata mafunzo hayo wakayaweke kwenye vitendo waliyojifunza kwa kuwapatia elimu wananchi kwenye maeneo yao.

“Kundi hili la wenyeviti wa serikali za mitaa ni kundi muhimu, mna watu wengi nyuma yenu, wapo karibu na watu na wana ushawishi, naamini mtafikisha elimu hii kwa wananchi",amesema.

"Na msiogope kwenda kudai fidia ili watoa huduma wetu hawa wasilale usingizi kwa sababu tusipokuwa tunawadai huduma hata haki zetu zinapokiukwa watalala usingizi. Tusipoamka na kuwasukuma huduma zetu zitazorota pia na serikali inataka kila taasisi iwajibike.Tudai fidia zile na wakiona tunadai fidia kila tunapokuwa tumekwazwa,wataamka na kuwajibika. Haki ni staki haihitaji kubembeleza ili upewe”,ameongeza Mhandisi Mmari.

Mwenyekiti wa EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga, Kudely Sokoine ameitaja miongoni mwa mifano ya malalamiko ya watumiaji wa huduma za maji na nishati ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wateja ni pamoja na ongezeko la bili za umeme na maji, kuunguliwa vyombo vya umeme na makazi,migogoro ya usomaji mita, Makampuni kushindwa kutengeneza miundombinu inayopitisha huduma na uharibifu unaotokea majumbani kutokana na maji machafu na hitilafu za umeme.

Malalamiko mengine ni ucheleweshaji wa kuunganishwa kwenye huduma husika kwa watumia huduma wapya wanaotaka kuunganishwa na huduma za umeme na maji, Watoa huduma kushindwa kutoa mwitikio wa kuridhisha kwa maswali au malalamiko kutoka kwa watumiaji/wateja na maswali kuhusu namna bili zisizo na mita zinavyoandaliwa na ukadiriaji viwango vyake.

Mweka Hazina wa EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga, Joseph Ndatala amesema mtumiaji wa huduma za maji na nishati ana wajibu wa kulipa Ankara kwa wakati, kutunza miundombinu ya huduma ili iweze kuwa endelevu huku akisisitiza kuwa Huduma bora ni haki ya mtumiaji wa huduma za nishati na maji.

Katibu wa EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga, Zezema Nyangaki Shilungushela amesema kazi ya EWURA CCM ni kutetea watumiaji wa maji na nishati ili kuelewa haki zao huku akizitaja huduma zinazodhibitiwa na EWURA ni Maji,bidhaa zitokanazo na petrol (petroli,mafuta ya taa na mafuta mazito), umeme na gesi asilia.

Amewashauri watumiaji wa nishati ya umeme kuwa wanapokuwa nyumbani watumie umeme muda unaotakiwa, kuwasha taa eneo walipo na kuepuka kumwaga mwaga maji ili kupunguza gharama

Mjumbe wa EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga, Jonathan Manyama amesema Mtumiaji wa huduma za maji na nishati ana haki ya kuhudumiwa kwa wakati na kwa mujibu wa miongozo,kanuni, sheria na bei ya halali zilizopitishwa na kutangazwa na mamlaka husika na kwamba ana haki ya kupata taarifa kuhusu huduma zinazotolewa mfano kusitishwa kwa huduma kutokana na matengenezo.

Afisa Huduma kwa Wateja Msaidizi wa SHUWASA, Masaka Kambesha amesema hivi sasa Mamlaka imeanza kutoa Bili za maji kila ifikapo tarehe 20 ya kila mwezi na wateja kutakiwa kulipia bili zao ndani ya siku 30 na kwamba wamekuwa wakituma bili kupitia namba za simu za wateja wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 25,000 mpaka sasa hivyo kuwaomba wale ambao hawajaunganishwa na huduma hiyo wafike katika ofisi za SHUWASA ili waanze kupata bili za maji kwa nji ya simu.

Nao wenyeviti hao wa serikali za mitaa wameishukuru EWURA CCC kuandaa semina hiyo ambayo imewajengea uelewa na kuahidi kwenda kutoa elimu hiyo kwa wananchi ili kujua haki na wajibu wao wanapotumia huduma za nishati na maji.
Katibu Mtendaji wa EWURA CCC Mhandisi Goodluck Mmari akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na EWURA CCC kuhusu haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za nishati na maji. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Mtendaji wa EWURA CCC Mhandisi Goodluck Mmari akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na EWURA CCC kuhusu haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za nishati na maji.
Katibu Mtendaji wa EWURA CCC Mhandisi Goodluck Mmari akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na EWURA CCC kuhusu haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za nishati na maji.
Katibu Mtendaji wa EWURA CCC Mhandisi Goodluck Mmari akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na EWURA CCC kuhusu haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za nishati na maji.
Mwenyekiti wa EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga, Kudely Sokoine akizungumza wakati wa semina ya Wenyeviti wa serikali za mitaa iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) Mkoa wa Shinyanga.
Katibu wa EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga, Zezema Nyangaki Shilungushela akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na EWURA CCC kuhusu haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za nishati na maji.
Katibu wa EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga, Zezema Nyangaki Shilungushela akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na EWURA CCC kuhusu haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za nishati na maji.
Mweka Hazina wa EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga, Joseph Ndatala akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na EWURA CCC kuhusu haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za nishati na maji.
Mjumbe wa EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga, Jonathan Manyama akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na EWURA CCC kuhusu haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za nishati na maji.
Mtoa Huduma kwa Wateja EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga Leonce Bizimana akizungumza wakati wa mafunzo kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa Manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na EWURA CCC kuhusu haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za nishati na maji.
Afisa Huduma kwa Wateja Msaidizi wa SHUWASA, Masaka Kambesha akitoa ufafanuzi kuhusu maswali ya washiriki wa semina hiyo.
Mwakilishi kutoka TANESCO Shaban Chein akitoa ufafanuzi kwa maswali yaliyoulizwa na washiriki wa semina hiyo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Miti Mirefu Manispaa ya Shinyanga, Nassor Warioba akiuliza swali wakati wa semina hiyo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitangili Manispaa ya Shinyanga Habiba Jumanne akiuliza swali wakati wa semina hiyo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Dome Manispaa ya Shinyanga Solomoni Nalinga Najulwa 'Cheupe' akiuliza swali wakati wa semina hiyo.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Busalala Nhelegani kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga Sophia Henerico Shitobelo akiuliza swali wakati wa semina hiyo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugwandege Manispaa ya Shinyanga , Amani Abdalah akiuliza swali wakati wa semina hiyo.
Katibu Mtendaji wa EWURA CCC Mhandisi Goodluck Mmari akifuatilia mjadala ukumbini
Wenyeviti wa serikali za mitaa wakiwa ukumbini
Mafunzo yanaendelea
Mafunzo yanaendelea
Wenyeviti wa serikali za mitaa wakiwa ukumbini
Mafunzo yanaendelea
Wenyeviti wa serikali za mitaa wakiwa ukumbini
Wenyeviti wa serikali za mitaa wakiwa ukumbini.

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments