" BIBI ANAYEDAIWA KUMUUA MJUKUU KWA KULA ELFU 2 AFIKISHWA TENA MAHAKAMANI SERENGETI

BIBI ANAYEDAIWA KUMUUA MJUKUU KWA KULA ELFU 2 AFIKISHWA TENA MAHAKAMANI SERENGETI
Kesi ya mauaji inayomkabili bibi anayeshitakiwa kwa kosa la kumpiga na kusababisha kifo cha mjukuu wake baada ya kutumia sh2,000 alizouza mkaa imeahirishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara hadi Februari 24 mwaka huu.

Kesi hiyo ya Mauaji namba 1/2022 kwa mara ya kwanza ilitajwa mahakamani hapo Januari 28,2022 ambapo mshtakiwa Nkwandu Kayenze(76)mkazi wa Kitongoji cha Bugerera Kijiji cha Natta wilayani hapa alisomewa shitaka la mauaji ya mjukuu wake na hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.

Ilidaiwa kuwa Januari 11 mwaka huu alimpiga mjukuu wake Matoja Deus (13) na kusababisha kifo chake kwa kosa la kutumia Sh 2,000 alizotumwa kuuza debe moja la mkaa mnadani Omahe kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Leo Alhamisi Februari 10,2022 mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Serengeti Adelina Mzalifu Mwendesha Mashitaka wa Jamhuri Paschal Nkenyenge amesema,jalada hilo limefika mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa wakati wakisubiri utaratibu mwingine,na kuahirishwa hadi Februari 24 mwaka huu.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments