WIZARA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA WATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya  Utawala na  Rasilimali watu Bi Veronica S. Nchango akiongea na watumishi wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya KAIZEN kwa watumishi ambao wamehamia katika Wizara hiyo na watumishi ambao hawakuwahi kupata mafunzo hayo kabla.  Mafunzo hayo yanatolewa kwa siku tatu  kuanzia  16 Februari 16, 2022 hadi Februari 18 2022 katika Ukumbi wa Chuo Cha Elimu ya Biashara CBE Jijini Dodoma. Bi.Veronica Nchango amemwakilisha Katibu Mkuu katika hafla  ya ufunguzi wa mafunzo hayo.

Na Doreen Aloyce, Dodoma

KATIKA Juhudi za kuendeleza uchumi wa Viwanda hapa nchini,Wizara  ya Uwekezaji,Viwanda na Biashara imeandaa mafunzo maalumu ya  KAIZEN kwa  watumishi wa Wizara hiyo lengo likiwa ni kuboresha utendaji kazi katika maeneo ya kazi jambo ambalo litaleta ufanisi mkubwa.

Aidha mafunzo hayo yenye kauli mbiu "KAIZEN kwa Tanzania ya viwanda shindani na maendeleo shirikishi"  yamelenga pia  watumishi waliohamia Wizara ya Uwekezaji na wengine ambao hawakuwahi kupata mafunzo hayo.

Akifungua mafunzo hayo ya siku tatu Mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na  Rasilimali watu (DAHRM)  kutoka Wizara ya  Uwekezaji,Viwanda na Biashara Bi Veronica  Nchango amewataka washiriki kuwa Chachu kuchangia kukuza maendeleo ya viwanda na kuongeza uchumi wa Nchi.

Amesema kuwa Serikali  inatagemea kupata matokeo yenye tija kwa Serikali kupitia mafunzo hayo huku akiwataka wakufunzi kuwafatilia kwa ukaribu ambao wamepata elimu kujua kama wanayofundishwa wanayafanyia kazi ili kuleta tija kwa Taifa letu na sio kuishia Kutoa mafunzo.

"Niwashukuru wale waliowezesha mafunzo haya wakiwemo Jaica ambao wamefadhili mradi huu ambao unalenga kuongeza tija na ubora Katika Sekta zote hivyo  niwaombe muwe wasikivu kwa siku hizi tatu mkitoka hapa muwe mmeiva "

"Tunapaswa kuwa kioo kupitia KAIZEN kuwa na mtazamo chanya ili Jamii ione matokeo ya kuendeleza maendeleo ya viwanda hapa nchini" amesema Mchango.

Janne Lyatuu Mkuu wa  Kitengo cha KAIZEN Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Janne Lyatuu ametumia fursa hiyo kuiomba Wizara kuwa mafunzo hayo yawe endelevu Nchi nzima.

"Tunaomba mafunzo yawe endelevu kwa watumishi wa Wizara na Nchi nzima na niwaombe wale wenye muamko wa kusoma masomo haya waelekee kwenye kuleta Mabadiliko kwa wizara.

Kwa upande wake Meneja wa Dodoma Semphao  Manongi amesema kuwa endapo wataitumia dhana ya Kaizeni itasaidia kubadilisha uchumi wa nchi .

"Endapo tukiifanyia kazi hii dhana na kuitekeleza kama inavyotakiwa tunaweza kufufua viwanda vyetu na kuliokoa Taifa letu " amesema Manongi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo hayo yataenda kuwajenga na kuwaongezea uelewa ambao utawasaidia kuinua uchumi wa Nchi kupitia viwanda.

Mkuu wa Kitengo cha KAIZEN  ( TKU) kutoka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bi. Janne Lyatuu akimkaribisha mgeni  rasmi  aweze kuongea na  watumishi wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya KAIZEN kwa watumishi ambao wamehamia katika Wizara hiyo na watumishi ambao hawakuwahi kupata mafunzo hayo kabla. Mafunzo hayo yanafanyika katika Ukumbi wa Chuo Cha Elimu ya Biashara CBE Jijini Dodoma.
Meneja wa SIDO Mkoa wa Dodoma Ndugu Semphao Manongi  akitoa mafunzo kwa  watumishi wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara katika hafla ya ufunguzi wa mafunzo ya KAIZEN kwa watumishi ambao wamehamia katika Wizara hiyo na watumishi ambao hawakuwahi kupata mafunzo hayo kabla .Mafunzo hayo yanafanyika  katika Ukumbi wa Chuo Cha Elimu ya Biashara CBE Jijini Dodoma.  Ndg.Semphao Manongi ni miongoni mwa   wakufunzi wanaotoa mafunzo ya KAIZEN kutoka katika taasisi zilizo chini ya Wizara  Uwekezaji, Viwanda na Biashara
Watumishi wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara wakifuatilia Mafunzo ya KAIZEN kwa umakini zaidi katika ukumbi wa Chuo Cha Elimu ya Biashara jijini Dodoma
Picha ya pamoja ya  watumishi wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ambao hawakuwahi kupata fursa ya kuhudhuria  mafunzo ya KAIZEN  kabla, wakiwa na mgeni rasmi aliyefungua mafunzo hayo Bi.Veronica S. Nchango  baada ya hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo yanayoendelea kutolewa  katika Ukumbi wa Chuo Cha Elimu ya Biashara CBE Jijini Dodoma kwa siku tatu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments