RAIS SAMIA AFUNGA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA NCHINI,ATAKA MAHAKAMA KUKOMESHA RUSHWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Sheria nchini yaliyofanyika katika Viwanja vya Chinangali Mkoani Dodoma leo tarehe 02 Februari, 2022. Picha na IKULU

**

Na Dotto Kwilasa-Malunde 1 Blog- DODOMA.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefunga kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini baada ya maadhimisho hayo kuzinduliwa Januari 23, 2022  na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Husein Mwinyi Jijini Dodoma.

Kufungwa kwa maadhimisho hayo kunaashiria kuanza kwa Kalenda mpya ya mahakama kwa Mwaka huu ambapo mbali na Rais Viongozi mbalimbali wamehudhuria wakiwemo wa Serikali,Viongozi wa Dini pamoja na Wananchi huku  yakienda sambamba na kaulimbiu isemayo zama za mapinduzi ya nne ya viwanda safari ya maboresho kuelekea Mahakama mtandao.

Akiongea kwenye maadhimisho hayo leo jijini hapa amesema licha ya juhudi nyingi zinazofanywa na mhimili huo katika kutenda haki bado suala la rushwa lipo na hivyo  kuitaka mahakama kuendeleza kulikemea vikali suala hilo.


Kutokana na hayo,Rais Samia amewataka Watendaji wa Mahakama Nchini kuendelea kutenda haki kwani bado kuna malalamiko kwa  baadhi ya wananchi kucheweleshewa haki na wakati mwingine kunyimwa kabisa haki hasa kwa wanawake wajane kuhusu masuala ya mirathi.


Aidha amesema Serikali itawaunga Mkono Kikamilifu Mahakama katika matumizi ya Teknolojia za kisasa za TEHAMA ili kukabiliana na uchumi wa kisasa katika kufanikisha lengo hilo  ambapo ni Lazima Kuboresha Sheria kwani Mapinduzi ya Viwanda yamesababaisha mabadiliko ikiwemo mfumo wa elimu za vyuo vikuu Wanaofundishwa kukabiliana na mapinduzi hayo kupitia mifumo hiyo.


Hata hivyo amesema wataliangalia suala la upungufu wa uhaba wa watumishi wa mahakama ikiwemo usafiri pamoja na vitendea kazi ili kuiwezesha Mahakama katika utendaji kazi wake pamoja na kufanya suala la  uwekezaji katika Mahakama mtandao.

Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania,Profesa Ibrahim Juma ameeleza  changamoto mbalimbali  zilizopo katika mhimili huo ikiwa ni pamoja na matumizi madogo ya uwekezaji  hasa katika suala la TEHAMA,upungufu wa watumishi pamoja na suala la akili bandia katika mahakama.


 Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jaji  Dk.Elieza Feleshi ametumia nafasi hiyo  kumwomba Rais Samia kuongeza bajeti kwa mwaka huu wa fedha ili kuchochea Katika kushughulikia mashauri yalifunguliwa kwa njia ya mtandao.

Amesema,mfumo wa mahakama mtandao huwezesha kuhifadhi kumbukumbu na kuongeza usalama wa mashahidi walio na hofu ya kujitokeza na kutoa ushahidi wao kwa usalama.

"Tunaahidi kuongeza uwazi  katika mpango wa mahakama na kuhakikisha kuwa mfumo huu unatumika katika ngazi zote za Mahakama nchini, faida za matumizi ya mfumo huo  ni kuongeza uwazi ikiwa ni pamoja na kurahisisha utendaji kazi kwa kutumia TEHAMA kwa kuwa taarifa zote muhimu za kufanyia kazi zinawekwa kiielektroniki, 

kuongeza ufanisi wa kazi, kuongeza kasi ya kufanya maamuzi kwa wakati, kupunguza matumizi ya karatasi na kudhibiti matumizi mabaya ya taarifa za kiofisi,"amesema


Mbali na mfumo huu, Mwanasheria mkuu huyo wa serikali ameeleza kuwa Mahakama pia ina mifumo kadhaa ya TEHAMA  ikiwemo  wa kusajili na kuratibu mashauri kwa njia ya Kieletroniki (JSDS), ‘TAMs’ na mingineyo yote ikilenga katika kumrahisishia mwananchi kupata huduma ya haki kwa wakati.

Naye Rais wa Chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) DK. Edward Hosea amesema ni wakati wa sekta ya sheria kujidhatiti kufanya maboresho ya utoaji haki hasa katika suala la utoaji taarifa sahihi kwa kutumia huduma mtandao pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi  juu ya ubongo bandia katika utoaji haki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Sheria nchini yaliyofanyika katika Viwanja vya Chinangali Mkoani Dodoma leo tarehe 02 Februari, 2022. Picha na IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali, Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu mara baada ya kuhutubia katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Sheria nchini yaliyofanyika katika Viwanja vya Chinangali Mkoani Dodoma leo tarehe 02 Februari, 2022. Picha na IKULU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. George Simbachawene mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma kwa ajili ya kushiriki katika Kilele cha Maadhimisho hayo leo tarehe 02 Februari, 2022. Picha ana Ikulu

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments