OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI YAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI WA MITANDAO YA KIJAMII

Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kanda ya Ziwa, Anna Masanja akizungumza wakati akifungua Kikao Kazi kati ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari vinavyotumia Mitandao ya Kijamii ‘Online Media Platforms’.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imekutana na Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari vinavyotumia Mitandao ya Kijamii ‘Online Media Platforms’ nchini kwa ajili ya kujadili na kutambua jinsi ya kuripoti taarifa za Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa vyombo vya habari vya mtandaoni (Online Media)  ili kuongeza weledi zaidi wanapoandika habari zao.

Kikao kazi hicho cha siku tatu kikishirikisha waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii kutoka Kanda ya Ziwa na mikoa mingine nchini kimefanyika leo Jumatano Februari 2,2022 katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Programu ya Kujenga uwezo endelevu wa kupambana na rushwa Tanzania - Building Sustainable Anti – Corruption Action Tanzania (BSAAT) kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza na Umoja wa Ulaya.

Akifungua kikao hicho, Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kanda ya Ziwa, Anna Masanja amesema kikao hicho kinalenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari kupitia mitandao ya kijamii juu ya utoaji wa taarifa za ubadhirifu na viashiria vya rushwa zinazotokana na taaifa ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

“Waandishi wa habari mitandaoni ni wadau muhimu na kwa kuzingatia ukweli huu ndiyo maana tumewaita hapa kwa ajili ya kupeana ujuzi na ufahamu wa masuala ya sheria zinazosimamia utekelezaji wa majukumu ya ofisi yetu sambamba na kukumbushana masuala muhimu katika kutekeleza jukumu lenu la kuwasilisha taarifa zinazohusu masuala ya ubadhirifu yanayoibuliwa na taarifa ya Ukaguzi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali”,amesema Masanja.

“ Imani yetu kuu ni kuwa mkielewa vizuri mtatusaidia sana katika kuwaelewesha wadau na wananchi kwa ujumla namna ya kusimamia rasilimali na fedha kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu. Na kupitia vyombo vyenu vya habari mtatusaidia sana katika kuchambua kwa ufasaha kwa kutumia lugha nyepesi ambayo kila mwananchi ataweza kuielewa vizuri na kufanya maamuzi sahihi ya kusimamia matumizi mazuri ya rasilimali za taifa”,ameongeza.

Masanja amesema hii ni mara ya kwanza kwa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kuhusisha waandishi wa habari kupitia mitandao ya kijamii pekee yaani Online Tvs, Blogs, kurasa mitandao ya vyombo vya habari (digital platforms) zenye wafuasi wengi mfano Twitter, Facebook na Instagram.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kanda ya Ziwa, Anna Masanja akizungumza wakati akifungua Kikao Kazi kati ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari vinavyotumia Mitandao ya Kijamii ‘Online Media Platforms’ nchini katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza leo Jumatano Februari 2,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kanda ya Ziwa, Anna Masanja akizungumza wakati akifungua Kikao Kazi kati ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari vinavyotumia Mitandao ya Kijamii ‘Online Media Platforms’ nchini

Mkurugenzi Huduma za Sheria - Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Elieshi Saidimu akizungumza kwenye Kikao Kazi kati ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari vinavyotumia Mitandao ya Kijamii ‘Online Media Platforms’ nchini
Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari vinavyotumia Mitandao ya Kijamii ‘Online Media Platforms’ wakiwa ukumbini.
Mratibu wa Programu ya BSAAT inayojengea Taasisi za Serikali uwezo wa kudhibiti Rushwa, Dkt. Bonaventure Baya akizungumza kwenye Kikao Kazi kati ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari vinavyotumia Mitandao ya Kijamii ‘Online Media Platforms’

Afisa Sheria Mwandamizi - Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Mratibu wa Programu ya BSAAT, Frank Sina akizungumza kwenye Kikao Kazi kati ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari vinavyotumia Mitandao ya Kijamii ‘Online Media Platforms’ nchini
Mkurugenzi Huduma za Sheria - Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Elieshi Saidimu akitoa mada kuhusu Mambo muhimu kuhusu ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwenye Kikao Kazi kati ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari vinavyotumia Mitandao ya Kijamii ‘Online Media Platforms’ nchini

Maafisa kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakiwa ukumbini
Washiriki wa Kikao Kazi kati ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Waandishi wa Habari kutoka vyombo vya habari vinavyotumia Mitandao ya Kijamii ‘Online Media Platforms’ wakipiga picha ya pamoja.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments