PASTA ALA SUPU NA KUWAPA WAUMINI KIDOLE CHAKE WAKILAMBE KAMA KOMUNYO

Video ya pasta mmoja akiwapa kondoo wake kidole chake walambe kama komunyo imezua ghadhabu kwenye mitandao ya kijamii.

Pasta huyo alikuwa akiwalambisha waumini kidole chake baada ya kula chakula aina ya eba na supu kwenye madhabahu.

 Eba ni chakula kikuu kinacholiwa sana katika ukanda wa Afrika Magharibi, hususan nchini Nigeria na Ghana.

Katika video hiyo, mtumishi huyo wa Mungu anaonyeshwa akichukuwa chakula hicho kutoka kwa mhudumu wa wageni kwenye upande wake kushoto.

 Kisha anaweka kidole kichafu ndani ya mdomo wa muumini mmoja kama komunyo na kukiosha katika beseni iliyokuwa imeshikiliwa na mwanamke mwingine katika upande wa kulia.

Mchungaji huyo mwenye utata alirudia utaratibu huo kwa washarika wote walipokuwa wakienda madhabahuni mmoja baada ya mwingine kupokea 'meza ya Bwana.' 

Si mara ya kwanza pasta huyo kugonga vichwa vya habari na matukio tatanishi anayowafanyia kondoo wake. 

Hivi majuzi alinaswa kwenye video akiwaogesha waumini wa kike kanisani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post