" WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AAGIZA ZAWADI ALIYOPEWA MKE WAKE IUZWE

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AAGIZA ZAWADI ALIYOPEWA MKE WAKE IUZWEWaziri Mkuu Kassim Majaliwa, alipotembelea soko la madini ya Tanzanite Mirerani na kushuhudia uchongaji wa madini hayo siku za hivi karibuni
**

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameagiza zawadi aliyopewa mke wake Mama Mary Majaliwa na mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na kampuni ya Tanzanite Forever Lapidary (T) LTD ambayo ni kidani cha Tanzanite iuzwe ili fedha zitumike kwa ajili ya kujenga bweni la wanafunzi wa wilaya ya Simanjiro.

Maelekezo hayo ameyatoa akiwa Mirerani wilayani Simanjiro alipohitimisha ziara yake ya siku nne kwenye mkoa wa Manyara ambapo licha ya kushukuru kwa zawadi hiyo ila akaagiza iuzwe kisha fedha zitakazopatikana zitumike kujenga bweni moja kwenye shule iliyopo Simanjiro.

Chanzo - EATV

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments