RAIS MWINYI ATUMA SALAMU ZA POLE VIFO VYA WATU 14, WAKIWEMO WAANDISHI WA HABARI




RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemtumia salamu za pole Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknonojia ya Habari, Nape Nnauye kufuatia ajali ya gari iliyotokea Wilaya ya Busega mkoani Simiyu na kusababisha vifo vya watu wakiwemo waandishi wa habari.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ametoa salamu hizo za pole kwa ndugu jamaa na marafiki pamoja na wadau wote wa habari.

Katika salamu hizo za rambirambi, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kusikitishwa na vifo hivyo na kuwasihi ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wadau wote wa habari kuwa na subira na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha misiba hiyo.

Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi, Amin.

Sambamba na hayo, Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu kuwaponya kwa haraka wale wote waliopata majeraha kutokana na ajali hiyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments