MVUA KUBWA KUNYESHA MIKOA 15 TANZANIA
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa itakayonyesha hii leo Januari 17, 2022, katika baadhi ya maeneo huku athari zinazotajwa kutokea ni pamoja na shughuli za uchumi kusimama na makazi ya watu kujaa maji.

TMA imeitaja mikoa ambayo itakumbwa na mvua hizo ni pamoja na Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Arusha na Manyara.

Aidha mvua hiyo pia itanyesha kesho Januari 18, katika mikoa 15 ya Mwanza, Kagera, Geita, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Dodoma, Arusha, Lindi, Mtwara, Mara na Singida. Huku Jumatano ya Januari 19 mvua hiyo ikitarajiwa kunyesha kwenye mikoa 12

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments