MTOTO MBARONI TUHUMA ZA KUUA MTOTO MWENZAKE TANGA
JESHI la polisi mkoani Tanga linamshilikia mtoto wa miaka (9) mkazi wa mji mpya Hale na mwanafunzi wa shule ya msingi Kichangani darasa la tatu iliopo wilayani Korogwe mkoani Tanga kwa kosa la mauaji ya Ally Khalifa Bakari (9) mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Kichangani mkazi wa Msalo Hale.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Safia Jongo amesema mauaji hayo yametokea leo Januari 28, 2022 majira ya saa nane mara baada ya wanafunzi hao kutoka msikitini.

Amesema tayari maafisa wa polisi wakiongozwa na mkuu wa upelelezi wilayani Korogwe wamefika katika eneo la tukio kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda Jongo amesema mwili wa marehemu umekutwa na majeraha mengi sehemu mbalimbali hivyo uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini kama tukio hilo limefanywa na mwanafunzi huyo pekee.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kichangani Riziki Selungato yeye anasema watoto hao waliruhusiwa muda wa saa sita na robo mchana ili waende msikiti kuswali wote wakiwa salama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post