MCHUNGAJI, MKEWE WAKAMATWA KWA KUWAFUNGIA NDANI WATU WENYE ULEMAVU



MCHUNGAJI mmoja aliyetambulika kama Curtis Keith Bankston (55) na mkewe Sophia Simm Bankston wamekamatwa na maofisa wa Polisi kwa madai ya kuwafungia ndani walemavu nane wa akili ndani ya nyumba yao katika eneo la Griffin huko Georgia nchini Marekani.

Wachunguzi wanasema kwamba wawili hao walidhibiti fedha za waathiriwa na mara nyengine kuficha matibabu yao. Madaktari waliitikia wito wa ripoti kwamba kulikuwa na mgonjwa ambaye alikuwa na mshtuko wa moyo tarehe 13 Januari.

Baada ya kubaini mlango uliokuwa ukielekea katika sehemu hiyo ya chini ya nyumba , maafisa wa masuala ya dharura waliarifu polisi , ilisema taarifa ya polisi.

Maafisa walisema kwamba , waliwapata walemavu wanane wenye akili tahira walio na umri kati ya 25 na 65 ambao walikuwa mara nyengine wakifungiwa na bwana Bankston na mkewe Sophia Simm Bankston.

Uchunguzi ulibaini wanandoa hao walikuwa wakikodisha nyumba hiyo kwa miezi 14 na kuitumia kama nyumba ya kuwatunza watu hao ambao polisi inasema walikuwa wamefungiwa kinyume na matakwa yao.

Wakati huohuo, maafisa walisema kwamba waligundua kwamba Curtis Bankston alikuwa akitumia nyumba hiyo kwa kisingizo cha kuwa kanisa na kudai kwamba yeye ni mchungaji. Yeye na mkewe bi Sim Bankston wameshtakiwa kwa kuwafungia watu kinyume na matakwa yao.

Idara ya huduma za watu walio na umri mkubwa iliitwa na kuwaweka watu hao katika mazingira mazuri ya kuwatunza, ilisema taarifa hiyo. Maafisa wa polisi wanatafuta haabari kutoka kwa wakazi wengine ambao huenda walikuwa na wapendwa wao katika nyumba hiyo.

Taarifa ya wakili wa Curtis Bankston iliotolewa kwa mshirika wa BBC, CBS ilisema kwamba alikana madai hayo dhidi yake na kudai kwamba zilitokana na habari zisizo za kweli zilizotolewa na polisi.


Taarifa ilidai kwamba kituo hicho hakikukuwa kundi la nyumba za kuwatunza walemavu , na badala yake kanisa ambalo limekuwa likitoa malazi kwa watu wasio na malazi .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments