MBUNGE APIGWA STOP KUINGIA BUNGENI BAADA YA KUGAWA PIPIMbunge mmoja mwanamke nchini Kenya amesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa siku moja kwa kosa la kusambaza pipi kwa wabunge wenzake wakati wa mijadala muhimu bungeni.

Mbunge huyo Fatuma Gedi (pichani) alijitetea kwamba kiwango cha sukari cha wabunge mwilini hushuka chini baada ya vikao virefu vya siku.

Fatuma alituhumiwa na mbunge Ndindi Nyoro kuwa anasambaza fedha za rushwa ndani ya Bunge la Kenya.

Nyoro alipotakiwa kutoa ushahidi wa tuhuma hizo za rushwa dhidi ya Fatuma alishindwa na Bunge likamsimamisha na yeye kwa siku mbili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments