MAMA AJITOLEA KUMZALIA MTOTO MWANAE


MAPYA yaibuka! Pichani Maree Arnold (54) kutoka Australia ameamua kumbebea mimba mwanae huyo wa kumzaa Meagan (28) hivyo kumzaa mjukuu wake wa kiume mwenye afya njema tarehe 13 mwezi huu.

Imekuwaje? Meagan akiwa na miaka 17 aligundulika kuwa hana mfuko wa uzazi(uterus) hiyo ina maana kwamba hata period haingii kila mwezi na kamwe asingeweza kuja kubeba mimba na kuzaa, hata hivyo licha ya changamoto hiyo lakini madaktari waligundua bado ovaries zake zinafanya kazi hivyo baadaye akiamua bado anaweza kupata mtoto wake mwenyewe (biological child) ikiwa atatokea mwanamke mwingine wa kumsaidia kumbebea mimba.

2015 akakutana na jamaa pichani ambaye kwasasa ni mumewe, jamaa alipojua changamoto za mkewe wakakubaliana watafute mwanamke wa kuwasaidia kuwabebea mimba (surrogate) ambapo alipatikana nchini Canada kupitia agency flani, mimba ilibebwa na surrogate lakini mtoto akiwa na wiki 21 akafariki kisha janga la corona lilipoingia ndio kabisa Meagan akaanza kukata tamaa maana ilikuwa ngumu hata kusafiri nje ya nchi.

Maree alipoona binti yake huyo hana furaha muda mwingi sababu ya kuamini hatakuja kupata mtoto wake mwenyewe maishani, akafanya utafiti kidogo na kuambiwa licha ya kuwa tayari yeye ana miaka 54 na alishazaa watoto 5 lakini bado anaweza kumsaidia kumbebea mimba mwanae huyo wa kumzaa.

Maree alienda hospitali kupandikizwa embryo (kiinitete) kilichotokana na yai la mwanae na mkwe wake, alipandikizwa mara tatu lakini zote haikufua dafu ikashindikana kwa mara ya nne ndio ikakubali.

Kwa umri wake wa miaka 54 Maree tayari alikuwa hedhi imeshakoma(menopause) hivyo kabla ya kupandikizwa mimba hiyo ilibidi madaktari wampe dawa za ku-reverse process ya menopause na kujaribu kuuboresha mfuko wake wa uzazi uweze kubeba mtoto tena.

Maree akizungumza amesema mimba hii ilimfanya achoke zaidi kulinganisha na miaka 22 iliyopita alipobeba mimba ya mwisho ya mtoto wake halisi, lakini amesema amejisikia fahari kumsaidia mwnaae na kama muda ungekuwa unarudi nyuma basi angejitosa kumbebea mwanae mimba ya mtoto mwingine.

Kwa upande wa Meagan kwasasa furaha yake hailezeki baada ya kufanikiwa kuitwa mama kwa mtoto ambaye ni damu yake, aidha, pia amemshukuru sana mzazi wake kumbebea mimba.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments