KIJANA ATUHUMIWA KUMUUA MPENZI WAKEMaafisa upelelezi nchini Kenya wamemkamata kijana aitwaye Brian Waweru mwenye umri wa miaka 25, kwa tuhuma za utekelezaji wa mauaji ya kinyama aliyoyafanya kwa mpenzi wake Everlyn Wanjiru (24), katika eneo la Ndenderu, Kaunti ya Kiambu.

Brian na Wanjiru kwa pamoja walikuwa wakimiliki saloon ya kiume huko Thindigua na wamekuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu kabla ya kuanza kutofautiana baina yao, mwezi Oktoba, mwaka jana.

Wakati anatekeleza mauaji hayo, Waweru alikuwa na kesi ya kumshambulia mchumba wake huyo katika Mahakama ya Kiambu na alikuwa nje kwa dhamana.

Baba wa Wanjiru ameeleza kuwa mtuhumiwa pamoja na familia yake, walimfuata mzee huyo na kumuoma wayamalize kifamilia badala ya mahakamani jambo ambalo familia zote mbili ziliridhia, lakini mahakama ilikataa, wawili hao kurejea tena kwenye mahaba yao tangu wakati wa sikukuu za mwisho wa mwaka (Desemba) kabla ya mauaji hayo kutokea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post