KATIBU MKUU WA CCM : MCHAKATO WA KUMPATA SPIKA MWINGINE BAADA YA NDUGAI KUJIUZULU UNAENDELEA

 


TAARIFA KWA UMMA

KATIBU MKUU WA CCM ATHIBITISHA KUPOKEA BARUA YA KUJIUZULU KWA SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel G Chongolo leo tarehe 06 Januari, 2022 amethibitisha kupokea barua ya Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb) ya kujiuzuru nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katibu Mkuu ameeleza kuwa mchakato wa kumpata Spika mwingine baada ya nafasi hiyo kubaki wazi unaendelea.

Imetolewa na;

Said Said Nguya
Afisa Habari 
Ofisi ya Katibu Mkuu 
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo ndani ya Bunge leo Alhamisi, Januri 6, 2022 kutokana na fukuto la kisiasa linaoendelea kufuatia kauli yake aliyoitoa kuhusu Rais Samia Suluhu kukopa Tsh trilioni 1.3.


"Naomba kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania kuwa leo Tarehe 6 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,uamuzi huu ni binafsi na hiari na nimeufanya kwa kuzingatia na kujali maslahi mapana zaidi ya Taifa langu,Serikali na Chama cha CCM", - Mhe.Job Ndugai 

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments