Monday, January 10, 2022
JAMAA AJIUA NJE YA KANISA IBADA IKIENDELEA
RAIA mmoja wa kaunti ya Homa Bay ameamua kujinyonga kwa kitanzi nje ya kanisa wakati ibada ikiendelea.
Joshua Odoyo Nyariera, mwenye umri wa miaka 23, anaripotiwa kujinyonga katika Kanisa la Oneno Nam Raha Msalaba, siku ya Jumamosi, Januari 8, dakika chache baada ya waumini wa kanisa hilo kuanza ibada ya Sabato.
Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, Odoyo aliwacha nyuma kijikaratasi akisema kuwa aliamua kujiua sababu ya kulemewa na madeni aliyoshindwa kulipa.
Marehemu ambaye alikuwa mhudumu wa Mpesa mjini Homa Bay, pia aliongeza kuwa alihofia kukamatwa na polisi na kufungwa jela ilihali hangeliweza kumudu gharama ya wakili wa kumwakilisha kortini.
Kulingana na mzee wa kanisa hilo, Benson Oyieng, marehemu alikuwa akiabudu nje ya kanisa kabla ya tukio hilo.
Oyieng alisema Odoyo pia alitoa maagizo ya namna alitaka mazishi yake yaandaliwe, akiamuru kuwa mwili wake kamwe usihifadhiwe mochari akitaka uteketezwe na kisha majivu yazikwe.
Mzee huyo aliwaomba waumini wa kanisa hilo kufunguka kuhusu changamoto zao kwa wenzao badala ya kujiua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Malunde 1 blog ni blog ya Kiswahili maarufu duniani kwa habari za Matukio, Siasa, Magazeti, Nyimbo za asili na habari za kusisimua.
No comments:
Post a Comment