CHELSEA YAZIDI KUPUNGUZWA KASI MBIO ZA UBINGWA EPL YATOKA SARE YA 1-1 NA BRIGHTON - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, January 19, 2022

CHELSEA YAZIDI KUPUNGUZWA KASI MBIO ZA UBINGWA EPL YATOKA SARE YA 1-1 NA BRIGHTONTIMU ya Chelsea imetoa sare ya 1-1 na wenyeji, Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumanne Uwanja wa The AMEX, Falmer, East Sussex.

Hakim Ziyech alianza kuwafungia wageni dakika ya 28, kabla ya Adam Webster kuwasawazishia wenyeji dakika ya 60 na sare hiyo ya nane ya msimu inazidi kuiondolea Chelsea matumaini ya ubingwa sasa kikosi cha kocha Mjerumani, Thomas Tuchel kikiachwa pointi 12 na mabingwa watetezi, Manchester City.

Chelsea inafikisha pointi 44 katika mchezo wa 23 nafasi ya tatu, nyuma ya Liverpool pointi 45 za mechi 21 na Man City pointi 56 za mechi 22, wakati Brighton imefikisha pointi 29 katika mechi ya 21 nafasi ya tisa.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages