CCM YAMPITISHA DKT. TULIA ACKSON KUMRITHI JOB NDUGAI USPIKA


Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), leo Alhamisi Januari 20, 2022 imempitisha Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kuwania nafasi ya uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kurithi nafasi ya Job Ndugai aliyejiuzulu.

Kikao cha Kamati Kuu ya CCM kimeketi leo katika Ukumbi wa White House jijini Dodoma na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambapo Dk. Tulia ameibuka kinara kati ya wagombea 70 waliojitokeza.


Akizungumza jijini Dodoma katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Shaka Hamdu Shaka baada ya kikao hicho amesema hatua inayofuata ni jina hilo kupigiwa kura na Caucas ya wabunge wa chama hicho.

Kikao hicho cha kamati kuu, kimekuwa na jukumu zito la kuwafyeka wagombea 69 kati ya 70 waliojitosa kwenye kinyanyany’iro hicho na kubaki na jina moja la Tulia ambalo litapelekwa katika kamati ya wabunge wa CCM ili kudhibitishwa.

Kamati ya wabunge wa CCM, itakuwa na jukumu la kumchagua na atakwenda kukiwakilisha chama kwenye uchaguzi wa spika utakaofanyika Februari Mosi, 2022, siku ya kwanza ya mkutano wa kwanza wa Bunge la sita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments