BARRICK YADHAMINI MKUTANO MKUU WA TAWOMA

Waziri wa Madini,Dk. Doto Biteko akihutubia wajumbe wa mkutano Mkuu wa 24 wa TAWOMA uliodhaminiwa na kampuni ya madini ya Barrick
**
Katika mwendelezo wake wa kufanya kazi na wadau mbalimbali, kampuni ya madini ya Barrick imedhamini mkutano wa 24 wa Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania (TAWOMA) mwaka huu uliofanyika mkoani Dodoma na kufunguliwa na Waziri wa Madini, Dk.Doto Biteko.

Mkutano huo ulihusisha na maonesho ya bidhaa za madini kutoka kwa wanachama wa chama hicho ambacho kilianzishwa mwaka 1992 kikiwa na malengo ya ni kuhamasisha Wanawake wengi kuingia kwenye Sekta ya Madini na kuwakomboa kiuchumi kupitia Elimu, Mitaji na Masoko.

Barrick imeeleza kuwa itaendelea kusaidia shughuli mbalimbali kupitia sera ya kusaidia huduma za kijamii ambayo imefanikisha miradi mbalimbali ya kuwakomboa wananchi kiuchumi katika maeneo yanayozunguka migodi yake pia inaendelea kuwezesha miradi ya afya na elimu sambamba na kufadhili progamu za kuwapatia wananchi elimu ya ujasiriamali na kilimo cha kisasa.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa TAWOMA wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko.

Wanachama wa TAWOMA walipata fursa ya kuonyesha shughuli zao

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post