ASKARI POLISI ALIYENASWA AKIPOKEA RUSHWA KWENYE MABASI AKAMATWATAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Iringa imethibitisha kumkamata askari wa usalama barabarani kwa kosa la kupokea rushwa kwenye mabasi maeneo ya Ipogolo manispaa ya Iringa Januari 18, 2022.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mkoani Iringa kamanda TAKUKURU mkoa wa Iringa,Domina Mukama alisema kuwa walimkamata Copro Steven Mchomvu akipokea rushwa kwenye mabasi ambayo yanapita katika barabara ya ipogolo.

Alisema kuwa picha ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zilipigwa na maafisa wa TAKUKURU mkoa wa Iringa mara baada ya kumkamata askari huyo wa usalama barabarani akipokea rushwa kutoka kwenye basi.

Mukama alisema kuwa polisi huyo bado anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Iringa na taratibu zote zikikamilika watatoa taarifa nini kitafanyika kwa mujibu wa sheria za nchi.

Alisema kuwa walimkuta na kiasi cha sh 150,000 pesa tathilimu ambazo alikuwa nazo mfukoni ambazo alikuwa akipokea rushwa kwa magari mbalimbali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post