CCM DODOMA YAWATAKA WANA CCM KUACHA USALITI, MAJUNGU NA ROHO MBAYA...'RAIS NI MMOJA TU AHESHIMIWE'


 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma,Dkt. Damas Mukkasa
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, Dkt. Damas Mukkasa

Na Dotto Kwilasa,Malunde 1 blog,Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma kimewataka baadhi ya wanachama na ambao sio wanachama wa chama hicho kuacha,usaliti,uzandiki, majungu,fitna na roho mbaya kwani Rais ni mmoja tu hivyo anatakiwa aheshimiwe.

Hatua hiyo imekuja kufuatia jana Rais Samia Suluhu Hassan kudai kwamba kuna baadhi ya wanachama wa chama hicho wamekuwa wakimsaliti katika suala la nchi kukopa.

Kupitia kauli ya Rais Samia, alisema lazima nchi ikope kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa madarasa kwakuwa fedha za tozo haziwezi kutekeleza mahitaji ya miradi hiyo.

Amesema mkopo ambao Serikali umeupata wa Sh trilioni 1.3 ni mzuri na haujawahi kutokea tangu nchi ipate Uhuru.

Akizungumza kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma leo Januari 5,2022, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, Dkt. Damas Mukkasa kuhusu kumpongeza Rais kwa hotuba yake aliyoitoa Januari 4,2022 Jijini Dare-es-Salaam baada ya kupokea taarifa ya Mpango wa maendeleo wa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19.

Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dodoma amemuomba Rais Samia kufanya kazi bila uoga na kuachana na baadhi ya watu ambao wana uchu wa madaraka.

Dkt. Mukassa ametoa wito kwa Wana CCM kuacha majungu,fitina na roho mbaya, kuacha kuharibiana kwani Rais ni mmoja na hivyo aheshimiwe.

Katika hatua nyingine amelaani makundi yanayowania Urais kwa mwaka 2025 kwani huo ni usaliti na tamaa na badala yake wamuunge mkono Rais katika utendaji kazi ili kuleta maendeleo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments