AHMED ALLY ATANGAZWA KUWA AFISA HABARI SIMBA SC


Aliyekuwa Mtangazaji wa  Azam TV Ahmed Ally leo Jumatatu Januari 3,2022 ameteuliwa kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano (Afisa Habari) katika Klabu ya Simba SC.

Kabla ya kutangazwa kuwa Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally alikuwa mtangazaji wa Azam TV, lakini kabla ya hapo aliwahi kufanya kazi kwa muda mrefu kwenye kampuni ya Sahara Media (Radio Free Africa na Star TV).

Kupitia ukurasa wa Facebook wa Simba SC wameandika:
"Ni kijana mchapakazi, mwenye uhusiano mzuri na watu wa aina zote, mtanashati na kubwa zaidi mapenzi yake kwa Simba hayapimiki.

Ahmed Ally karibu kwenye klabu ya maisha yako kuwatumikia Wanasimba kama Afisa Habari na Mawasiliano. #NguvuMoja

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments